aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, August 19, 2013

FILAMU ya kimataifa iliyoandaliwa Swahilihood na kwa ushirikiano wa nchi 6 inayojulikana kwa jina la Going Bongo imekamilika

 Filamu ya Going Bongo iliyogharim M. 450 za Kibongo.

FILAMU ya kimataifa iliyoandaliwa Swahilihood na kwa ushirikiano wa nchi 6 inayojulikana kwa jina la Going Bongo imekamilika mwezi wa nane, kwa sasa watayarishaji wapo katika mikakati ya kufanya uzinduzi ambao utatangazwa wakati wowote, akionge na FC mmoja wa watengenezaji wa filamu hiyo Nick Marwa amesema kuwa filamu hiyo ni kazi ambayo inaweza kuwa ni ya kwanza kwa kushirikisha watalaam kutoka nchi mbalimbali. 

George Mboya from KenyaGeorge Mboya mpiga picha wa Kenya akiwa kazini
Ernest RwandalahDr. Erenest akimfanyia mtu upasuaji.
“Filamu ya Going Bongo ni kazi nzuri ambayo imewakutanisha watu wa mataifa mengi kulingana na fani za filamu, lakini pia wasanii wakubwa wa filamu wa Tanzania na nje ya nchi wameigiza pamoja na wasanii wa ndani ni hatua moja ya ukuzaji wa tasnia ya filamu Bongo, huku kukiwa na changamoto ya makapuni mengine kuwekeza pesa nyingi katika filamu,”anasema Nick. 
Nchi zilizoshirikiana katika utayarishaji wa filamu hiyo ni Tanzania, Italy, Kenya, Marekani, UK, Turkey na filamu ya Going Bongo ilianza kurekodiwa Marekani katika jiji la Los Angeles, California na kuja kumaliziwa Tanzania wasanii walioshiriki katika filamu hiyo ni Ernest “Napoleon” Rwandalla kinara wa filamu, Ashley Olds huyu kutoka Marekani.

Sauda Simba Kilumanga Sauda Simba mwigizaji katika filamu ya Going Bongo.
Evance Bukuku , Sauda SimbaWaigizaji wa filamu ya Going Bongo Evance Bukuku na Sauda Simba.
mcdonald haule ernest napoleondar Mwandishi wa filamu akiwa na Mcdonald Haule katika utayarishaji wa filamu hiyo.
Wengine ni Emanuella Galliusi kutoka Itali na Nyokabi Gethaiga kutoka Kenya, kwa hapa nyumbani kuna waigizaji wakubwa kama Ahmed Olutu “Mzee Chilo”, McDonald Haule, Sauda Simba Kilumang , na mtangazaji mahiri wa Redio , Evans Bukuku ambaye pia ni mchekeshaji kutoka Redio Choice Fm. 
Watayarishaji wa filamu ya Going Bongo ni Nick Marwa, Ernest Napoleon, Bryan Ronalds, mswada umeandikwa na Ernest Napoleon Rwandallah na Gregory Zyment wapiga picha ni mwanadada Leslie Bumgarner kutoka Marekani akisaidiwa na George Mboya kutoka Kenya, Filamu imeongozwa na Dean Ronalds. 
Kulingana na makampuni ya usambazaji kununua filamu kwa kiwango cha chini inawezekana ikawa ni vigumu kuweza kununua filamu hiyo ambayo bajeti yake ya utayarishaji pekee ni milioni 450 za Kitanzania, filamu hiyo inatarajiwa kuonyeshwa Toronto Canada na baadae katika nchi zote washirika katika kutengeneza. Pia unaweza kuangalia Trailer kwa kupitia www.vimeo.com/71947975 

No comments:

Post a Comment