BAADHI ya mawaziri na polisi wametajwa kuwa ni wateja wakubwa wa wanawake wanaouza miili yao, maarufu kwa jina la Changudoa.
Hayo yameelezwa jana na Jukwaa la Wanaharakati Wanawake Vijana (YFF), walipokuwa wakiwasilisha ujumbe wao kwa njia ya sanaa ya ngonjera, katika tamasha la 11 la Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) linaloendelea eneo la Mabibo jijini Dar es Salam.
Wanaharakati hao wanawake vijana, walisema tatizo liko kwenye jamii ambayo inawahukumu changudoa bila kujiuliza kuwa wateja wao ni kina nani.
‘’… jamani hebu tuulizane, kwani changudoa mteja wake nani? Kwa taarifa yako, mawaziri, wabunge na mapolisi wamo; na hii ni changamoto kwa jamii,’’ walisema wanaharakati hao.
Akizungumza na Tanzania Daima baada ya kutoka jukwaani, kiongozi wa wanaharakati hao, Aisha Kijavala, alisema wameamua kutoa ujumbe huo kwa washiriki wa tamasha hilo ili jamii ijue wateja wa changudoa hao.
Alisema wateja hao wakiacha kununua ngono, pia wanawake wanaouza miili yao, wataacha kujiuza.
source:gumzo
No comments:
Post a Comment