STAA wa filamu za Kibongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’, hivi karibuni walinaswa wakipigana mabusu hadharani na mumewe Gardina Dibibi, nyumbani kwa mwanamuziki Isabella Mpanda, huku watu wakiwatumbulia macho.
Jack ndiye aliyetangulia kufika na saa mbili baadaye Dibibi aliwasili ndipo walipoanza kupigana mabusu huku watu wakiwaangalia lakini wao hawakuonekana kujali.
“Mmh! Sasa huu uzungu umepitiliza maana kama ni mahaba hapa yamefika mwisho, tangu walipowasili wao ni kupiga mabusu tu,” alisikika mmoja wa waalikwa wa sherehe hiyo.
Jack na Dibibi walifunga ndoa hivi karibuni na watu wengi wamekuwa wakitabiri kwamba wawili hao hawatadumu ndani ya ndoa hiyo.
Hivyo kitendo chao cha kupigana mabusu hadharani ni sawa na kuwaonesha wasiowatakia mema kwamba wanapendana kwa dhati.
Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ na mumewe Gardina Dibibi wakibusiana.
Tukio hilo lilitokea maeneo ya Makumbusho, jijini Dar ambapo Isabella alikuwa akimfanyia sherehe ya kutimiza miaka hamsini mama yake mzazi, Slavina Mpanda ambapo aliwaalika Jack na mumewe.Jack ndiye aliyetangulia kufika na saa mbili baadaye Dibibi aliwasili ndipo walipoanza kupigana mabusu huku watu wakiwaangalia lakini wao hawakuonekana kujali.
“Mmh! Sasa huu uzungu umepitiliza maana kama ni mahaba hapa yamefika mwisho, tangu walipowasili wao ni kupiga mabusu tu,” alisikika mmoja wa waalikwa wa sherehe hiyo.
Jack na Dibibi walifunga ndoa hivi karibuni na watu wengi wamekuwa wakitabiri kwamba wawili hao hawatadumu ndani ya ndoa hiyo.
Hivyo kitendo chao cha kupigana mabusu hadharani ni sawa na kuwaonesha wasiowatakia mema kwamba wanapendana kwa dhati.
No comments:
Post a Comment