Kanisa la Evangelistic Assemblies of God (EAGT) linatarajia kuuanza mwezi ujao kwa machungu mapya kabisa huku yale ya kuaga dunia kwa aliyekua Askofu wake mkuu Askofu Moses Kulola yakiwa hayajapoa.....
Kanisa hilo linatakiwa kusimama mahakamani mwezi ujao Oktoba 1 kujitetea ili waumini wake wasiondolewe kwenye kanisa la Bugando ambako askofu Kulola amezikwa.
Shauri la kesi hiyo lenye nambari 121/2013 lilifunguliwa mwaka huu kabla ya kifo cha Askofu Kulola .Kwa mujibu wa maelezo ya Askofu Mkuu wa TAG Dkt. Barnabas Mtokambali , kesi hiyo ni ya kudai kanisa la Bugando na ni mwanzo wa tu katika kudai mengine mengi.
Hili ni kaburi la Askofu Dr.Moses Kulola lililojengwa katika kanisa la EAGT Bugando. Pichani ni Rais Jakaya Kikwete alipoongoza maelfu ya wakazi wa Mwanza na mikoa mbambali katika mazishi ya Askofu Dr.Moses Kulola |
EAGT inatetewa na wakili Deocles Rutahidurwa wa Rwelu Attorney,Mwanza
Kwa mujibu wa nyaraka za TAG makanisa mengine yaliyoko kwenye orodha inayotakiwa EAGT wayaachie ni pamoja na yale yaliyopo Tabora, Dar es Salaam,Mbeya,Arusha ,Shinyanga,Tanga,Mwanza,Morogoro,Pwani,Singida,
Kilimanjaro, na maeneo mengine nchini.
Kwa Dar es Salaam makanisa yanayotakiwa na TAG ni pamoja na kanisa la Temeke ambako mwili wa wa marehemu Kulola uliagwa kwa mara ya kwanza kabla ya kusafirishwa kwenda Mwanza.
Katibu mkuu wa Kanisa la EAGT Mch.Brown Mwakipesile
Akielezea namna ambavyo kanisa la EAGT wamejiaandaa na changamoto hiyo, katibu mkuu wa Kanisa la EAGT Mch.Brown Mwakipesile amesema kwamba:
"Ikiwa Yesu alipelekwa mahakani sisi ni kina nani hata tuogope kushitakiwa,,sisi kama EAGT tupo tayari kwa chochote ambacho Mungu ataruhusu kitupate''
Upya wa kesi hiyo hiyo iliyofunguliwa na TAG baada ya kupita miaka 21 tangu makanisa hayo yagawanyike kutoka Assemblies of God (AG) na kuwa Tanzania Assemblies of God na Evangelistic Assemblies of God ni ishara kwamba kwa sasa TAG ina mtazamo mpya na kusudio thabiti la kuyadai makanisa hayo chini ya Askofu mkuu wa TAG Barnabas Mtokambali tofauti na maaskofu waliotangulia.
Askofu Mkuu wa TAG Barnabas Mtokambali |
Mapema mwezi huu wa September , Askofu Mkuu wa TAG Barnabas Mtokambali ilieleza alitoa kauli ifuatayo akielezea msimamo wa kanisa lake.
"Mila za kiafrika mtu akizikwa pale pale panakuwa kwake. Sasa tukasema kama tukikaa kimya hili likatokea baadae huko mbele tutasema nini ,.. tutajibu nini kwa sababu kanisa sio langu kanisa ni la general Council ..
"Mimi nawajibika kama mwenyekiti wa bodi ya wadhamini kwa wachungaji wote. Halafu sisi tutaondoka watakuja watoto hapa na wanataka kuchukua kanisa lao ambapo tayari kuna kaburi pale.Tusipokuwa makini watu wakachinjana hapo baadae.
"Lakini nawaambieni ukweli hakuna mtu aliyefurahia kama mimi kwa mzee kulola kuzikwa Bugando .Mimi nimefurahi sana na naomba muandike hivyo ndugu waandishi, nimefurahi sana Mzee kulola kuzikwa Tanzania Assemblies of God Bugando. (TAG ).
"Mzee kwa Heshima zote ameanza kazi Tanzania Assemblies of God mwaka 1968 , mzee akaombwa na EAGT uongozi. Kwa busara yao kubwa na nzuri wameona alipoanzia ndio apumzishwe, amerudishwa nyumbani amerudishwa nyumbani baba yetu .
"Mimi kama TAG na kama mwenyekiti wa bodi ya wadhamini lengo letu ilikua ni kuweka records sawasawa kwa ajili ya sasa na vizazi vijavyo kuzuia maafa makubwa yanayoweza kutokea baadae.
"Lakini haikua nia yangu kuzuia Mzee Kulola kuzikwa pale . Hata kesho tutakaporudishiwa lile jengo na kupewa umiliki kwa asilimia 100, mtu akitaka kuja kumuondoa mzee Kulola nyumbani mimi nitaweka stop order usimuondo."
-Baraka Samson wa mjap blog.
No comments:
Post a Comment