Sister feki baada ya kunaswa akikusanya fedha.
Akipekuliwa mabegi yake nyumbani alipokuwa akiishi.
POLISI mjini Narok nchini Kenya wanamshikiria mwanamke mmoja aliyenaswa akiwa na mavazi ya kitawa akikusanya fedha kutoka kwa watu wenye mapenzi mema akidanganya kuwa ni sister. Mwanamke huyo alikuwa akikusanya misaada ili aweze kurudi katika konventi alipotokea mpaka hapo aliposhutukiwa kuwa hakuwa mtawa. Alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na vitambulisho kadhaa. Mpaka ananaswa, sister huyo alikuwa amewatapeli watu kadhaa na anatarajiwa kufikishwa mbele ya sheria kesho.
Habari / Picha: KTN
No comments:
Post a Comment