aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, August 19, 2013

WATUHUMIWA WA DAWA ZA KULEVYA JNIA KUJIELEZA MBELE YA TUME....


 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JNIA)

MKURUGENZI wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JNIA), Moses Malaki, amesema watuhumiwa wa njama za kupitisha kilo 150 za dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine, watasimamishwa kazi wakati wowote kuanzia leo kabla ya kupewa nafasi ya kujitetea kwenye tume itakayoundwa kuwachunguza.
Hatua hiyo inatokana na agizo la Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, kutaka wote waliohusika na njama hizo kuchukuliwa hatua za kisheria. Malaki ambaye awali alionyesha kushangazwa na kiasi kikubwa cha dawa hizo kupita, alisema utaratibu unakamilika wa kuundwa tume na kuwasimamisha kazi wahusika.
“Baada ya tume kukamilika na kupewa hadidu rejea, tutawaita mmoja mmoja kwenye kujieleza, hapo tutajua kama wahusika watakuwa na hatia au la,” alisema.
Alisema baada ya kumaliza kazi, tume itatoa maelekezo kwa Serikali kinachotakiwa kufanyika. Katika hatua nyingine, jalada la mtuhumiwa wa dawa za kulevya aliyekamatwa JNIA Alhamisi iliyopita, akiwa na kete 84 na misokoto 34 ya bangi linapelekwa kwa Mwanasheria wa Serikali leo.
Kamanda wa Polisi Vikosi cha Viwanja vya Ndege nchini, Deusdedit Kato, alisema jana kuwa wameshakamilisha upelelezi na kwamba, wanasubiri maelekezo kutoka kwa Mwanasheria Mkuu.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa JNIA mwishoni mwa wiki iliyopita, akiwa katika harakati za kusafirisha dawa hizo kwenda nchini Italia kupitia Zurich, Uswisi. Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, kumekuja ikiwa ni siku moja baada ya Dk Mwakyembe kufanya ziara ya kushtukiza JNIA kukagua utendaji. 
CHANZO: www.mwananchi.co.tz

No comments:

Post a Comment