aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, August 3, 2013

WANAUME WAWILI WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA TISHIO LA UBAKAJI KUPITIA MTANDAO WA TWEETER NCHINI UINGEREZA..

 
Wanaume wawili wameshikiliwa na polisi kwa tuhuma za kutishia kumbaka mwanaharakati Cariline Criado-Perez kupitia ukurasa wa twitter.

yote hayo yalianza kutokana na kampeni ya kutaka kuwekwa picha ya mwanamke kwenye noti ya pound 10 ya uingereza iliyokuwa ikifanywa na Perez.

Masaa machache baada ya picha hiyo kupigwa, mwanaharakati huyo alishambuliwa kwa tweets za matusi na vitisho vya kumbaka na kumuua nyumbani kwake vilivyosambaa huku zikiambatana na adress ya mahali anapoishi.

 
"vitisho vikubwa sana, huku wakielezea kwa undani kitakacho tokea, na kulikua na vitisho vya kubaka na kuua." amesema Perez.

Huku akielezea kuwa alikuwa akipokea takribani tweet moja ndani ya dakika moja, Perez aliendelea kupokea tweets za kumshambulia kwa siku kadhaa kutoka kwa watu wasiojuikana (anonymos) ambao alikuwa akiwa block badala yake wanafungua akaunti mpya.

No comments:

Post a Comment