aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, August 19, 2013

WANASWA NA MENO 210 YA TEMBO....


MAOFISA wa Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, wamekamata meno 10 ya tembo yenye uzito wa kilo 45.5 yenye thamani ya Sh milioni 39.31. Meno hayo yalikamatiwa katika eneo la Mzombe Darajani, Kata ya Kidodi, Tarafa ya Mang'ula, Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro yakiwa katika maandalizi ya kusafirishwa. 
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alisema kukamatwa kwa meno hayo, kumetokana na taarifa iliyotolewa na raia mwema, kuwa kuna gari litapita eneo hilo likiwa limebeba meno ya tembo.

Baada ya kupata taarifa hizo, alisema kwa kushirikiana na maofisa wa Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa, waliweka mtego na kufanikiwa kukamata gari lenye namba za usajili T199 AQP aina ya Mitsubish Fuso, likiwa na meno hayo yaliyokuwa yamefichwa kwenye magunia ya mchele.

Kutokana na tukio hilo, alisema watu wawili wanahojiwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa na baada ya upelelezi kukamilika, watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Kamanda Shilogile aliwasisitizia wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na maofisa wa hifadhi kutoa taarifa pindi wanapokuwa na taarifa za kuibwa kwa nyara za Serikali.

Naye, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa, Nitalis Uruka, alisema meno hayo 10 ya tembo ni sawa na tembo watano.

Alisema meno hayo yenye uzito tofauti tofauti, yana uzito wa kilo 45.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kikosi cha Kuzuia Ujangili, Kanda ya Mashariki, Faustine Masalu, aliwataka wananchi kukabiliana na vitendo hivyo vinavyozidi kuongezeka.

"Katika historia hapa nchini, kuna maeneo yalikuwa yakitambulika kutokana na kuwa na wanyamapori wengi, lakini kwa sasa hawapo na yamebaki majina peke yake. Hivyo basi, jamii inapaswa kuendelea na jitihada za kukabiliana na ujangili nchini kwa lengo la kulinda rasilimali za nchi kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo," alisema Masalu.

No comments:

Post a Comment