aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, August 17, 2013

WAISLAMU WASALI CHINI YA ULINZI MKALI WA ASKARI...


 Mbwa wa polisi akiwa kazini jana kulinda amani 

 Ulinzi mkali jana uliimarishwa jijini Dar es Salaam baada ya kuwepo kwa tetesi kwamba waumini wa Kiislamu wataandamana kupinga kitendo cha Jeshi la Polisi kumuweka mahabusu Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda.Baadhi ya waumini walikuwa wameonyesha kukasirishwa na kitendo cha polisi kumwondoa Sheikh Ponda Hospitali ya Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) na kumuweka Gereza la Segerea.Kiongozi huyo alikuwa amelezwa MOI kwa madai ya kupigwa risasi begani akiwa mjini Morogoro. Hata hivyo, akiwa bado anatibiwa MOI, Jumatano alisomewa shtaka la uchochezi akiwa kitandani na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Tumaini Kweka akidaiwa kutenda kosa hilo katika maneo mbalimbali ya nchi kati ya Juni 2 hadi Agosti 11, mwaka huu.Kutokana na fununu za baadhi ya waumini kupanga kufanya maandamano, ulinzi uliimarisha maeneo mbalimbali ya jiji hususan misikiti ambayo inadaiwa wanasali wafuasi wake Msikiti wa Mtambani Waumini katika Msikiti wa Mtambani jana waliswali swala ya Ijumaa katika usimamizi mkali wa magari matano ya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).Hata hivyo, hali katika mazingira ya msikiti huo ilikuwa ni tulivu huku waumini wakisikiliza kwa makini kila kinachosemwa na viongozi wao, huku taratibu za ibada zikiendelea kama kawaida licha ya kuwepo kwa ulinzi mkali.Mapema kabla ya kuswali swala ya Ijumaa ambayo iliswaliwa saa saba za mchana, gari tano za kikosi cha kutuliza ghasia zenye askari waliovalia kivita na zana za kazi ikiwemo bunduki, yalikuwa yameegeshwa mbele ya lango kuu la msikiti huo, kitu kilichofanya litolewe tangazo msikitini hapo la kuwataka Waislamu kuja kuswali bila kuogopa vitisho vya magari hayo.Saa 5:18, lilisikika tangazo kutoka msikitini hapo ambalo lilisema, “Njooni msikitini msiogope vitisho vyao, hatutafanya vurugu lakini kama wanataka kupambana na sisi waje na tutapambana nao,” ilisikika sauti ya mtoa tangazo ndani ya kipaza sauti.Baada ya swala magari ya askari yalipungua na kubaki magari matatu ambayo hadi saa 9:45, bado yalikuwa yameweka kambi upande wa pili wa barabara kwenye eneo ulipo msikiti huo.Wakati wa ibada waumini hao walionyesha hisia zao baada ya kusomwa dua ya zaidi ya saa moja na nusu kama ambavyo hufanya kwenye swala ya alfajiri, na kilio kikatanda msikiti mzima yaani kwa upande wanawake na wanaume
 SOURCE: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment