aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, August 18, 2013

WAFANYAKAZI 120 ZANTEL WADAIWA KUFUKUZWA KAZI.KAMPUNI YASEMA WAMEMALIZA MKATABA....

WAFANYAKAZI 120 wa kampuni ya simu za mkononi ya Zantel kutoka Zanzibar wako hatarini kufukuzwa kazi.
Akichangia bajeti ya Wizara ya Mawasiliano na Miundombinu hivi karibuni,Mwakilishi wa Wete mwezi uliopita, Asaa Othman Said alisema nyaraka za wafanyakazi zinazoagiza kufukuzwa tayari zimeandaliwa baada ya Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo kusema hapendi kufanya kazi na Wazanzibari kwa sababu ni wavivu.

Aliiomba Wizara kuingilia kati kuhakikisha maslahi ya Wazanzibari yanalindwa na kuchukua hatua kuzuia wafanyakazi hao kufukuzwa.

Nimekasirishwa na kauli ya CEO wa Zantel hasa baada ya kusema I dont like Zanzibaris because are vey lazy (siwapendi Wazanzibari kwa wavivu), alisema Asaa.

Asaa alisema siku za nyuma aliwahi kuonya hatari ya kampuni hiyo kuhamishiwa Tanzania Bara kwa kisingizio cha kufuata soko kubwa zaidi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee alikiri hilo na kusema amefanya mazungumzo na uongozi wa Zantel kuhakikisha hilo halitokei.

Aidha alisema Waziri anaeshughulikia na ajira, Haroun Ali Suleiman nae amefanya mazungumzo na uongozi wa Zantel kuhusu sakata hilo, lakini hakuweza kutoa ufafanuzi kwa kuwa wakati huo hakuweko barazani.

Mzee alisema atahakikisha maslahi ya Zanzibar kutoka ndani ya kampuni hiyo yanalindwa na kumuonya Mtendaji mpya wa kampuni hiyo kutohamisha kodi kuipeleka Tanzania Bara.

Nilimtaka ahakikishe kile kinachofanywa na Mtendaji anaeondoka na yeye anakifanya na asijaribu kuhamisha kodi kupeleka Tanzania Bara, alisema.

Mzee aliwahakikishia Wawakilishi kumuachia yeye suala hilo na kwamba atalishughulikia kwa nguvu zote.

Hata hivyo, Mwanasheria wa kampuni hiyo, Salum Taufiq alikanusha akisema hakuna mfanyakazi aliefukuzwa kazi isipokuwa wafanyakazi 113 wamemaliza mkataba ambao uliokuwa muda wa miezi sita.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Taufiq alisema kampuni ina mikataba ya kudumu na ya muda kwa mujibu wa sheria za ajira, kutokana na hali hiyo wafanyakazi hao ambao waliokuwa walinzi wa minara baada ya kumaliza mkataba Disemba 31 hawakupewa mkataba mwengine.

Aidha alisema lengo la kampuni ni kubakia na wafanyakazi ambao watakuwa wanahusika na shughuli za msingi za mawasiliano, lakini pia haina maana ya kukiuka sheria na haki za mtu yoyote.

Pia alisema kesi hiyo ipo mahakamani hivyo ni vyema kusubiri maamuzi ya mahakama.    

No comments:

Post a Comment