aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, August 6, 2013

TANZIA,MWANAFUNZI HUYU WA CBE DODOMA AFARIKI DUNIA


MAREHEMU    RESTUTA  MAYUMA

Ni masikitiko makubwa kwa wanafunzi wa Chuo Cha 
Elimu ya Biashara (CBE)  kampasi ya Dodoma  kwa 
kumpoteza mwanafunzi mwenzao  Bi. Restuta Mayuma 
ambaye alifariki tarehe  05/08/2013 (Jumatatu) mnamo mishale 
ya saa kumi na moja jioni.

 Hata hivyo mwanafunzi huyo  alikuja dodoma kwa lengo
 la kufaya mitihani yake ( katika kipindi hiki ambacho wanafunzi 
wa Chuo cha CBE  wamekuwa wakiendelea kufanya mitihani yao 
ya Special pamoja na ile ya Supplimentary.

Marehemu Restuta, Alikuwa anasoma Diploma , kozi ya 
Uhasibu (Accountancy) , ambapo alianza masomo ya
 Diploma mwaka wa masomo 2011/2012 na alitakiwa kuhitimu  
Elimu yake  ya Diploma  mwaka 2012/213.Lakini  kwa kipindi 
hiki alikuja  chuo kurudia mitihani yake ya Diploma  I  .

Akizungumza  na blog hii Rafiki wa karibu sana na
 Mwanafunzi
 huyo (Marehemu Restuta)  alisema  Marehemu alikuwa
 anasumbuliwa na homa za hapa na pale (Malaria)  hali ambayo
 ilipelekea  mpaka kutokea kwa kifo chake.

 Tayari Mwili wake umesafirishwa leo kuelekea  Mkoani 
Dar es salaam eneo la BUNJU  kwa ajili ya shughuli za Mazishi 
ambapo  mwili huo umesafirishwa na Gari la Chuo (CBE)  Kwa 
kuambatana na  WARDEN, Mashauri Machunde (Mwanafunzi CBE) 
 pamoja na baadhi ya ndugu wa marehemu waliokuwepo mkoani 
Dodoma.



 Akizungumza kwa njia ya simu, Bw. Mashauri Machunde 
 (Mwanafunzi  CBE)  amewataka wanafunzi wote wa CBE 
wanaoishi jijini Dar es salaam kijitokeza katika mazishi ya  
Mwanafunzi huyo   yanayotarajiwa kufanyika   kesho  nyumbani 
kwao "Bunju " Kwa kupanda magari yaendayo Bunju na kushukia 
eneo la Bunju "A" kituo  kinaitwa Shule au Hospital
 (Uliza kwa Mzee  Mayuma  karibu na Shule ya Sekondari Fanaka)

No comments:

Post a Comment