aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, August 6, 2013

HUWEZI AMINI,HUU NDIO UTAJIRI WA MAJUMBA YA KIFAHARI YA MRISHO NGASA,MAGARI YA KISASA.

SASA ni miaka nane tangu aanze kucheza soka ya 
ushindani mwaka 2005 katika klabu ya Kagera 
Sugar ya Bukoba, lakini kwa namna alivyopanga 
vyema karata zake, Mrisho Khalfan Ngasasa anafurahia
 maisha ya mpira. Huwezi kumuita tajiri, lakini huwezi 
kuacha kumpa heshima miongoni mwa wachezaji wa
 kizazi chake, kwamba amewaacha mbali. Amecheza klabu
 nne katika Ligi Kuu tu, baada ya Kagera Sugar ni Yanga 
SC mwaka 2007 hadi 2010, Azam 2010 hadi 2012 na sasa 
amerejea Jangwani.
Ikulu; Ngassa akiwa katika nyumba yake ya Mwanza. Hii ndiyo nyumba bora zaidi kati ya zote na itakuwa maskani yake akistaafu soka. Ipo eneo la Bwiru.
 Hakuna maslahi makubwa aliyopata Bukoba, zaidi 
alikuwa anatafuta njia ya kutokea katika soka ya 
Tanzania na tangu Yanga SC hadi sasa unaweza 
kusema Mrisho ametumia kipindi hicho kuchanga 
vyema karata zake. Anamiliki nyumba tano, tatu 
zipo Mwanza na mbili Dar es Salaam- na ana gari 
nane, wakati huo huo akaunti yake wakati wote 
ikiwa ‘imefulia sana’ ina Sh. Milioni 20. Akiwa bado 
anategemea soka kama ajira yake, Ngassa 
amekwishaanza kujipanga kwa maisha ya baada 
ya soka na katika mahojiano na BIN ZUBEIRY
 wiki hii anasema anafanya biashara ya usafirishaji na kilimo.
Ngassa akiwa na bibi na babu
Ngassa katika kaburi la shangazi yake
Ngassa na watoto wake

“Katika gari zangu nane, gari tatu za biashara, 
mbili ni zangu mwenyewe za kutumia, moja ya 
shughuli za nyumbani wakati wote na mbili 
nimewagawia baba na mama kila mmoja na yake,”.
 Ngassa anasema baada ya kustaafu soka atajitanua
 zaidi kibiashara, kwani ndoto zake ni kutoka kuwa
 mwanasoka nyota hadi mfanyabishara mkubwa.   
 “Mimi ujuzi wangu ni soka. Baada ya hapa 
sitegemei kurudi shule kusomea chochote, 
nitafanya biashara. Nimekwishaanza 
kufanya utafiti wa biashara za kufanya,”.
 “Sitarajii kufanya biashara za kibishoo za 
kuigana igana sijui kufungua saluni au maduka
 ya nguo. Mimi nitafanya biashara kubwa na 
siku moja nitatatambulika kama mwanasoka 
wa zamani na mfanyabiashara mkubwa, 
tayari nina mashamba kama matatu, hapo
 nazungumzia kilimo, ambacho kwa sasa ni  
biashara kubwa,”anasema Ngassa.
Nyumba nyingine ya Mwanza
Moja ya gari za kutembelea za Ngassa ikiwa katika nyumba ya Dar es Salaam, Yombo.
Nyumba ya Bwiru ni marumaru tupu
Ngassa akiwa na watoto

Pamoja na kufanikiwa uwanjani na katika maisha katika upande 
wa kuwekeza, Ngassa hakuwa mvivu pia katika ujenzi wa 
familia, hadi sasa akiwa na umri wa miaka 25, ana watoto wawili,
 ambao ni Farida (5) na Farkhiya (3). Ngassa anawajali sana 
watoto wake na wote anaishi nao mwenyewe, ingawa ametengana
 na mama yao, kwa sasa akihakikisha wanapata malezi bora,
 ili wakue vizuri. Baada ya kumaliza kuitumikia timu ya soka ya
 taifa ya Tanzania, Stars katika mechi za kuwania kucheza 
Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), 
Ngassa ameenda likizo Mwanza tangu Jumatatu na
 anatarajiwa kuripoti kazini, Yanga SC Jumapili. Ngassa
 alijaribu sana kuibeba Stars akitoa krosi ya bao lililofungwa
 na Amri Kiemba na kukaribia kufunga mara mbili, lakini 
Tanzania ikalala 3-1 mbele ya Uganda mjini Kampala na 
kutolewa CHAN.  Amekubali matokeo na kwenda kusalimu wazazi, 
ndugu, jamaa na marafiki baada ya mwaka mzima wa kuwa
 kazini Dar es Salaam. Akiwa huko, Ngassa alitembelea bibi 
na babu zake, ndugu, jamaa na marafiki hadi vijijini na pia 
kuzuru kaburi la shangazi yake aliyefariki mwezi mmoja 
uliopita yeye akiwa ametingwa na majukumu ya kitaifa. 
Gari la Ngassa la Mwanza
Gari lingine la Ngassa 

Ngassa aliwatemebelea watoto na kuwazawadia mipira ili 
wacheze soka, akiwahamasisha kujibidiisha na wao watakuwa 
kama yeye siku moja, kwani hata yeye aliaanzia kama wao.
 Mjini Mwanza, Ngassa ni kama mfalme, anapendwa mno
 kutokana na mfumo wake wa maisha, siku zote ni kijana 
mwenye nidhamu, adabu na utii- na asiyesahau asili yake. 
Likizo yake hii ya sasa amekwenda hadi msikitini kufuturu na 
waumini wenzake wa dini ya Kiislamu na kufanya ibada ya
 sadaka. Anatakiwa dua njema tu na watoto hadi wazee, wake 
kwa waume na hakuna ajabu akiendelea kuwa mwanaoska
 nyota Tanzania.
SOURCE:BIN ZUBEIRY

No comments:

Post a Comment