aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, August 4, 2013

Taarifa kamili kuhusu Watanzania waliovamiwa na kujeruhiwa nchini Ugiriki



Katika mitandao hivi karibuni zilionekana picha za watanzania wawili waliovamiwa na kupigwa  vibaya  Ugiriki.



Picha hizo hazikuwa na maelezo ya kutosha  na hatimae zilizusha maswali mengi yaliyokosa majibu muwafaka.
Jumuiya ya watanzania ugiriki baada ya kikao cha tume maalum inapenda kutoa  taarifa kamili ifuatayo:
1.   Waliovamiwa ni Makamu Mwenyekiti  bw. SALUM MSELEM  na Mhazina bw. SAID MOHAMED SAID  maarufu kwa jina la NURAMO(CHIDI)  NDUGU HAWA SI WAKIMBIZI, NI WATANZANIA HALISI.
2.   Mabwana hao walikuwa wanapita kwenye garden usiku  wa Jumatano 01/08/2013 kuelekea makwao,wakitokea  kwenye kikao muhimu ofisini .      Karibu na  garden hiyo kulikuwa na wezi waliokuwa wanajaribu kuvunja gari iliyokuwa imeegeshwa.Wezi hao walijishuku kama Salum  kawagundua wakamfuata kwa vitisho na kuanza kumpiga. Wakati huo lilitokea kundi lao jingine la watu wasiopungua  kumi wakaanza kumkimbiza Chidi ambaye alijitahidi kukimbia hadi  kufika chini ya nyumba anayoishi Salum(umbali wa mita 50)  huku akipiga kelele na hapo waliendelea kumpiga.Kelele za Chidi kwa bahati zilisikika na mke wa Salum  ambae nae alipiga kelele za kuomba msaada zilizowafanya  wakimbie na kumwacha Chidi akiwa hoi.
3.   Ndugu zetu tuliwafikisha hospitali  na tulitoa ripoti polisi  wanaoendelea na uchunguzi ambao hadi wakati huu tunapoandika maelezo haya HAKUNA TAARIFA ZOZOTE CHANYA  ZA KUWAKAMATA WAHUSIKA.
4.   Uongozi wa jumuiya unashindwa kutamka  kuwa wezi hawa wana uhusiano na kile kikundi maarufu kinachochukia na kuwavamia  wageni.Hatuna ushahidi.Bali tuna imani kubwa walikuwa ni vibaka toka nchi jirani.
5.   Tumeamua kuutaarifu ubalozi na vyombo vyote vya habari vilivyokuwa vimetumiwa taarifa za awali za tukio hili.
6.    Mwisho jumuiya yetu inatangaza bila kusita:                                         
VIONGOZI WETU HAWAKUFANYA BAYA LOLOTE  LILILOSABABISHA WAVAMIWE NA KUPIGWA. TUPO PAMOJA NAO KWA HALI NA MALI.
Ahsanteni                                                                            
Kny
TUME MAALUM YA JUMUIYA.
(Kayu Ligopora)
Source: Michuzi
1094591_10201494658909673_2108620625_o

No comments:

Post a Comment