MKANDA mzima wa askari bandia wa Kikosi cha Usalama Barabarani (trafiki), James Juma Hussein (45) aliyekamatwa saa 1:30 asubuhi ya Agosti, 14, 2013 maeneo ya Tabata Kinyerezi Mnara wa Voda, jijini Dar es Salaam akiwa ndani ya sare zake za kazi, umepatikana....
Kwa nini James alikamatwa? Asubuhi hiyo, afisa mmoja wa trafiki mwenye cheo cha ukaguzi alikuwa akipita eneo hilo kwenda kazini, alipomwona James alisimamisha gari, akashuka kwenda kumsalimia.
Lakini alishangaa kuviona vifungo vya shati lake ni vya kawaida (vya polisi vinatakiwa kuandikwa police force yaani ‘jeshi la polisi’), akamtilia shaka.
Afisa huyo Alimkamata ‘askari feki’ huyo mkazi wa Kimara Matangini, Dar na kumfikisha kwenye Kituo cha Polisi Stakishari, wilayani Ilala, Dar akafunguliwa jalada namba STK/RB/15305/2013 KUJIFANYA ASKARI ili taratibu za kisheria zichukuliwe juu yake.
Ndani ya kituo cha polisi, James alihojiwa haya: Askari: Wewe mtu wa wapi?
James: Mnyamwezi wa Tabora.
Askari: Una muda gani ukijifanya trafiki?
James: Wiki moja sasa.
Askari: Hii kofia ya polisi uliipata wapi?
James: Nguo nyeupe juu ya kofia niliitengeneza kienyeji, krauni, tepe za usajenti na mkanda ni za shemeji yangu alikuwa polisi Tabora, ni marehemu, alikuwa akiitwa Shaban.

James aliwaambia polisi kuwa suruali nyeupe ya kitrafiki aliishona mtaani lakini kamba ya filimbi na kizibao cha kung’ara vilikuwa vya polisi.
Askari: Uliwahi kuwa polisi?
James: Niliwahi kupata mafunzo ya upolisi katika Chuo cha Polisi Moshi (CCP) mwaka 1990-91 lakini nilifukuzwa kazi kwa sababu nilikwenda muziki. Nilirudi Tabora nikawa mkulima na mke wangu na mtoto mmoja ambao wote sasa ni marehemu.

Ndani ya nguo za kitrafiki alizokuwa amevaa James, alikutwa na suruali ya bluu na fulana ya kijani.
James alisema njaa ndiyo iliyomfanya ajifanye trafiki na ‘kuwapiga mikono’ madereva, hasa wa daladala ili anapowakuta na makosa kwenye magari yao ajipatie chochote.
Kamishina wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova amethibitisha kukamatwa kwa polisi huyo feki
No comments:
Post a Comment