aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, August 16, 2013

Mwanamke billionea afariki dunia.


Watu wengi mtakuwa mnaifahamu brand ya 
Zara maarufu sana kwenye dunia ya fashion, 
lakini watu ambao wako nyuma ya brand hii 
wanaweza wasiwe maarufu. Rosalia Mera 
ambaye hadi anafariki alikuwa na utajiri wa 
dola billioni 6.1 ambazo zinatokana na kuwa 
mmoja ya waanzilishi wa brand ya Zara akiwa
 na mme wake Amancio Ortega mwenye utajiri 
wa dola billioni 57.
Vyanzo vya habari vinasema kwamba mama huyu 
alikuwa likizo na mwanae ambapo alipatwa na 
ugonjwa wa uliotajwa kama “Brain hemorrhage”, 
baadaye alifariki dunia. Rosalia Mera akiwa na 
umri wa miaka 11 aliacha shule na baadae walianza
 kutengeneza magauni wakiwa nyumbani kwao na 
mme wake Amancio Ortega na hapo ndiyo mwanzo
 wa Zara. Rosalia Mera raia wa Hispania amefariki 
akiwa na miaka 69.

No comments:

Post a Comment