Mwalimu Bridgette Miller ameshitakiwa kwa madai ya kufanya mapenzi na mwanafunzi wake wa kiume ndani ya chumba cha darasa lake,Awali mwalimu huyo aliamua kufanya mapenzi mwanafunzi huyo ndani ya gari kwenye eneo la maegesho ya magari Walggreens ndipo alipoona haitoshi na kuamua kumpeleka darasani.
Bridgette Miller alishitakiwa kwa kosa la ubakaji baada ya kudaiwa kufanya mapenzi na mvulana huyo mwenye miaka 17 kwenye shule ya Chicago Vocational Career Academy.
Miller, mwenye miaka 39, anatuhumiwa kufanya mapenzi na mwanafunzi huyo nyuma ya Walgreens huko South Side mnamo Machi 17 na kisha kufanya mapenzi tena na mvulana huyo ndani ya chumba cha darasa Machi 22.
Miller alidaiwa kumwomba mwanafunzi mmoja namba ya simu ya mkononi ya mwenzake na kisha kutuma meseji za simu kwa mwanafunzi huyo, kwa mujibu wa nyaraka za mahakama zilizochapishwa kwenye gazeti la Chicago Sun-Times.
Wakati wa kusikilizwa kesi hiyo Ijumaa, jaji aliamuru dhamana yake iwe Dola za Marekani 150,000. Miller alipotafutwa kwa njia ya simu, haikujibiwa.
Miller anaishi eneo la West Side mjini humo na ana watoto watatu kwa mujibu wa mtandao wa ABC7.
Kwenye tovuti ya shule hiyo, Miller anaelezewa kama mwalimu wa teknolojia ya tiba. Anatarajiwa kupanda tena kizimbani Agosti 29, mwaka huu.
Shule hiyo inalenga katika kuwapatia wanafunzi fursa 'halisi za kazi' ambazo zitawasaidia kuwa mahiri kwenye taaluma walizochagua kusomea.
No comments:
Post a Comment