aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 15, 2013

LAANA...BABA AMBAKA BINTI YAKE NA KUZAA NAE WATOTO...


Aziza Kibibi alikuwa na umri wa miaka minane tu wakati baba yake - Mwongozaji wa Tuzo za muziki za MTV - alipoanza kumbaka.

Alipofika miaka 10, somo ambalo Aswad Ayinde alikuwa akimfundisha binti yake 'jinsi ya kuwa mwanamke' likabadilika na ubakaji wake wa mara kwa mara ukazaa watoto watano kutokana na makosa ya kujamiiana kwa kisingizio cha kujaribu kutengeneza damu 'halisi'.

Kwa namna ya ajabu mwanamke huyo jasiri, ambaye sasa ana miaka 35, ameolewa na anaendesha biashara inayoshamiri ya uokaji, alizungumza hadharani kuhusu maisha yake ya utoto yaliyojaa kiwewe wiki hii kwa mara ya kwanza.

Kibibi alielezea maisha yake ya utoto kwamba yalianza katika hali ya kawaida. Aliishi na mama yake na baba kwenye ghorofa ya tatu ya jengo moja huko Paterson, New Jersey, huku babu na bibi yake wahamiaji kutoka Jamaica wakiishi ghorofa ya chini.

Kibibi alikuwa akisomea nyumbani lakini bado aliruhusiwa kucheza na watoto wa jirani. Pale familia yake ilipoongezeka na kufikisha watoto wanane wakahamia kwenye nyumba kubwa zaidi katika jengo hilo.

Hapo ndipo Kibibi akaanza kukua kiasi cha baba yake kuanza kumtazama kwa jicho la matamanio.

"Aliniambia nilikuwa wa kipekee. Mwanzoni, ilikuwa ni katika kunifundisha jinsi ya kuwa mwanamke," alisema. "Wakati huo alianza kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mimi, aliendelea kutumia nguvu zaidi na zaidi. Pale nilipoanza kupigana naye, alinipiga. Alinipa vitisho vingi mno."
Baba yake akaanza kubadilika, na kuitawala mno familia kimabavu. Aliwahamisha kutoka kwenye nyumba ya babu yao na kuwapeleka kwenye nyumba nyingine huko Paterson kabla ya kuwahamishia Eatontown huko Southern New Jersey. Watoto hao walikuwa wakiruhusiwa tu kutazama televisheni kwa muda mchache mno, na hakuna ambacho kilielezea asili ya maisha ya familia.

Dawa za kisasa zilipigwa marufuku katika nyumba hiyo, na alimweleza mkewe kwamba uhusiano wake na Kibibi ulikuwa katika kumtibia ukurutu.

Kibibi hakuwa pekee ambaye Ayinde alikuwa akifanya naye mapenzi. Alikuwa na mwanamke wa makamo - mwanasheria wa Manhattan ambaye alizaa naye watoto wawili - na pia alikuwa akimdhalilisha kijinsia mmoja wa dada zake Kibibi.

Alijiita mzee wa mitala na nabii. Familia yake ilikuwa ikiruhusiwa kumwomba Mungu lakini wanaweza tu kufanya hivyo kupitia kwake.

"Alisema dunia ilikuwa ikielekea ukingoni, na angebaki yeye tu na watu wake na kwamba alikuwa amechaguliwa," mkewe wa zamani, Beverly Ayinde alitoa ushahidi kwenye kesi moja mwaka 2010. Alisema alikuwa akijaribu kutengeneza damu yake 'halisi' kwa kuzaa na binti zake mwenyewe.

Pale mtoto wa kwanza wa Kibibi alipozaliwa bila matatizo, Ayinde alitumia kigezo hicho kama uthibitisho na kuendelea kumbaka msichana huyo hadi kumpa ujauzito.

Watoto waliofuatia hawakuwa na bahati hivyo.

Mabinti wawili waliofuatia waliozaliwa kutokana na baba yake waligundulika na ugonjwa wa phenylketonuria (PKU) ambao huzuia mwili kuweza kuvunja amino acid. PKU inaweza kusababisha kuharibika ubongo na kifafa.

Dk Anna Haroutunian, mtaalamu wa PKU ambaye aliwatibu watoto wa Kibibi, alisema hakika wamepata ugonjwa huo sababu ya uzao baina ya wazazi wa nasaba moja.

Katika miaka hiyo, Kibibi amekuwa akikumbwa na shinikizo la kutoroka. Aliweza tu kulala sababu ndoto zake zilikuwa nzuri kuliko maisha halisi.

"Nilikuwa na ndoto ya kukimbia. Niliwaza kuwachukua kaka na dada zangu wote - mmoja wa dada zangu alikuwa mtoto, na nilikuwa nikimlea - nilikuwa na mawazo ya kuota matiti na kupata maziwa na kukimbia nao mahali fulani," alisema.

Pale alipokuwa mtu mzima na mmoja wa watoto zake wa kiume alipougua, hatimaye akapata hamasa kumpeleka hospitalini wakati Ayinde alipokuwa amekwenda mjini kwa safari ya kibiashara.

Lakini hakuwa akijua jinsi ya kuongea na madaktari na mfanyakazi wa jamii akaingia, akaitaarifu Idara ya Vijana na Huduma za Familia.

Pale Ayinde aliporejea kutoka safari yake ya kibiashara aligadhibika, na kutishia kumrejesha kwa nguvu mtoto wake kutoka hospitali.

Huduma za Watoto waliingia kabla hajachukua uamuzi huo na kuwaweka katika nyumba tofauti.

Baada ya hapo Kibibi, mama yake na dada yake walimtoroka Ayinde wakati akifanya harakati za kuwarejesha nyumbani watoto wake.

Akipambana kuwarejesha watoto katika himaya yake pia Kibibi aliwezeshwa, na kubadili maisha yake baada ya udhalilishaji. Sasa anaishi huko East Orange, New Jersey pamoja na mumewe.

Alirejea shule na atamaliza shahada yake ya sanaa kwenye Chuo cha Essex County mwaka huu. Pia anaendesha biashara yake ya uokaji na siku moja anapanga kuanzisha mgahawa.

Kibibi na dada yake mwishowe wameamua kufungua mashitaka dhidi ya baba yao mdhalilishaji. Walichelewa kufungua mashitaka kutokana na kutokuwa na uhakika wa athari ambazo zingeweza kuwapata watoto wao.

Ameeleza hadharani stori yake kwa matumaini ya kuweka utofauti kwa wote waliopitia maisha kama yake.

"Badala ya kuwa uzoefu niliokuwanao, pengine hii imeniimarisha. Kile kisichotusambaratisha kinatufanya tuwe imara zaidi."


No comments:

Post a Comment