SERIKALI imesema mtandao wa majangili wanaoua tembo
mkubwa wenye watu walio na uwezo kifedha ambapo wapo ndani
na nje ya nchi .Siri hiyo ilifichuliwa Dar es Salaam jana na Waziri
wa Mali Asili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, wakati
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukutana na
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii
.Alisema tayari Serikali ina majina ya mtandao unaojihusisha na biashara ya ujangili wa meno ya tembo na baadhi yao wapo pia wafanyabiashara wakubwa waliopo ndani na nje ya nchi."Tayari majina tunayo ya mtandao wa watu wanaojishughulisha na ujangili wa meno ya tembo huu ni mkubwa ambao una pesa nyingi, hauna tofauti na ule wa dawa za kulevya,"alisema
Alisema sio kwamba wameshindwa kufanya kazi bali wanaendelea
kupata taarifa na wameandaa operesheni hai itakayosaka wale
wote ambao wanahusika na ujangili huo.Aliongeza kuwa
wanaendelea kufuatilia nchi inayonunua meno hayo ambapo
nchi zilizopo Bara la Asia ni miongoni mwa zinazo husikana
biashara hiyo.Ali sema siorahisi ku shinda vita hiyo kwa
kutumia vyombo vya habari.
"Mnajua hii ni vita kubwa na ni waambie kuwa vita hii huwezi
kushinda kwa kutumia vyombo vya habari, hivyo Watanzania
kuwe ni na amani na tunajitahidi kuhakikisha tunamaliza tatizo
hili,"alisema.Katika hatua nyingine,alisema
mfumo wademokrasia uliopo unachangia kurudisha nyuma
jitihada mbalimbali zinazofanywa, kwani watu wakikamatwa na
kupelekwa mahakamani kesho yake wanaonekana mtaani.
Alisema wanaobainika kufanya biashara hiyo ya ujangili hata
Polisi wamo na wengine wameshafukuzwa kazi na wengine
kusimamishwa, hivyo hizo zote ni jitihada za Wizara
yake.Naye Mwenyekiti wa kamati hiyo John Lembei alisema
kuwa kamati yake imeiomba Serikali kuondoa kodi ya asilimia
tatu ambayo ilipitishwa na bunge kwa ajili ya mfuko wa
maendeleo ya utalii na asilimia kumi ambayo yalikuwa
yanawasilishwa Serikalini kwani inachangia kuondoa huduma za
jamii zilizokuwa zikitolewa kwenye jamii inayozunguka hifadhi
hizo.
Alisema kamati imeomba serikali kama kweli wanataka kuendeleza sekta ya utalii basi kodi hiyo ifutwe vinginevyo hifadhi hazitakuwa salama na ujangili utaongezeka kwa kiasi kikubwa."Hifadhi hizi za TANAPA na ngorongoro ilikuwa miradi ya kusaidia jamii inayowazunguka kwa kuwajengea shule, hospitali, maji, pamoja na huduma zinginezo hivyo kutokana na bunge kupitisha kodi hiyo wameondoa huduma hizo,"alisema Lembei.
No comments:
Post a Comment