aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, August 4, 2013

Mbwana Samatta kwenye headlines tu Mbwana Samatta kwenye headlines tu




Samatta
Yawezekana Taifa Stars ikawa haifanyi vizuri kwenye
 michuano ya kimataifa kiasi cha kuwa chini kwenye 
chati za soka barani Afrika na duniani kwa ujumla 
lakini jina la Taifa hili limekuwa likitajwa na lina 
uhakika wa kutajwa katika level za juu za soka barani
 afrika, hii ni kutokana na makubwa yanayofanywa
 na kijana mwenye umri wa miaka 21 raia wa 
Tanzania ambaye ni Mbwana Samatta .
Mchezaji huyu ambaye anacheza nafasi ya
 ushambuliaji amekuwa akifanya vizuri sana 
kwenye klabu yake ya Tp Mazembe ya Nchini
 Congo DRC kwenye michuano ya kimataifa na 
amekuwa na mchango mkubwa sana kwenye 
michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika .
Samatta alifunga bao moja kwenye mechi 
iliyochezwa jana kati ya timu yake ya Tp 
Mazembe na FUS Rabat ambapo Mazembe
 ilishinda 3-0 na mpaka sasa Samatta amekuwa 
akifunga kwenye mechi zote nne za michuano
 hiyo ambazo Mazembe imecheza hali inayomfanya
 awe na nafasi kubwa ya kuwa mfungaji bora wa
 michuano hiyo wakati ikimalizika baadaye mwaka huu.
Mbwana Samatta akiwa anasaini Autograph za mashabiki wa soka Ivory Coast ambao walivutiwa na uwezo wake wakati wa mazoezi ya Taifa Stars nchini humo.
Mbwana Samatta akiwa anasaini Autograph za 
mashabiki wa soka Ivory Coast ambao walivutiwa
 na uwezo wake wakati wa mazoezi ya Taifa Stars
 nchini humo.
Samatta ambaye Mazembe ilimsajili toka Simba 
Sports Club ya Tanzania ameendelea kuipeperusha
 vyema bendera ya Tanzania na amekuwa na rekodi 
nzuri sana ya kufunga karibu kila mechi ambayo 
anacheza kwenye klabu hiyo .
Samatta amefanya watanzania wengi kuwa na
 shauku ya kufahamu matokeo ya timu ya Tp 
Mazembe ambapo mara zote watu huuliza timu 
hiyo imeshinda au la na baada ya kuuliza hivyo 
huuliza tena Samatta amefunga mangapi kwa kuwa 
wana uhakika juu ya uwezo wake na rekodi yake ya
 kuzifumania nyavu.
Ubora wake umemfanya kuishi maisha ya kistaa
 akiwa nchini Kongo ambapo mashabiki wa Mazembe wanampenda kiasi cha kutaka kupiga naye picha kila 
wamwonapo mtaani na wakati mwingine kutaka 
kusukuma gari lake wanapoliona.

No comments:

Post a Comment