aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 15, 2013

MAKALA: SABABU KWANINI FRANK RIBERY NDIO MCHEZAJI ANAYESTAHILI KUTWAA TUZO YA MWANASOKA BORA WA ULAYA



Tuzo ya mchezaji bora wa ulaya ni nafasi nyingine ya 
ulimwengu wa soka kumtunza mchezaji bora kwenye 
mchezo wa soka barani ulaya. Tuzo hii haipaswi 
kufuata matakwa na mapenzi ya vyombo vya 
habari na kwa sababu hiyo tuzo hii safari haipaswi
 kwenda nchini Spain bali Ujerumani. 



Listi ya waliostahili na kusahaulika 
Tuzo za namna hii hukufanya ujiulize ubora wa mchezo
 huu hivi sasa. Listi ya wanasoka wanaoitwa bora haipo 
sawa. Kupuuzwa kwa wachezaji wanaocheza mchezo wa
 kuzuia unaonyesha kuna tatizo kwenye mchezo wa soka la 
kisasa. Kipaji binafsi, marudio ya vipande vya mechi na 
magoli ndivyo vitu ambavyo ulimwengu wa soka la kisasa
 na hizi tuzo za namna hii zinachoangalia katika kutoa 
ushindi wa mchezaji fulani. Labda hii ni kwa sababu ulimwengu
 wa sasa hutazami kiundani mchezo mzima.

Labda kwa sababu hii ndio maana mabeki na 
wachezaji kama  Carrick na Busquets mara nyingi
 wamekuwa wakichukulia poa bila kupewa heshima 
wanayostahili na mashabiki ambao wametekwa na
 vipande vya mtandao wa YouTube. Katika zama hizi 
za ukuaji wa teknolojia na mitandao ya kijamii 
inaonekana wazi kuna ukuaji mkubwa wa idadi ya 
mashabiki waitwao 'highlight fans'.

Hizi tuzo pia zimeanza kuwa tuzo za ushindani wa 
umaarufu. Kwa maana hiyo ndio maana wachezaji 
wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo hiyo ni 
 Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na mwanzoni alikuwepo
 pia Gareth Bale! Wote watatu walicheza vizuri msimu 
uliopita lakini ni Messi peke yake aliyeshinda japo kombe
 moja, La Liga.  
Kuna wachezaji wengi wazuri ambao inawezekana
 waliotoa mchango mkubwa kustahili kuwemo kwenye 
Top 10 ya wachezaji bora wa ulaya - ambao walimzidi 
hata Bale; wachezaji kama Marco Reus, alifanya vitu 
vikubwa kwenye michezo yenye ushindani kumzidi Bale. 
Juan Mata pia, alikuwa ndio mchezaji bora wa Chelsea
 msimu uliopita, kwangu mie inawezekana kumzidi hata 
Van Persie katika premier league. 
Na pia vipi kuhusu wachezaji kama Javi Martinez, Arturo 
Vidal na Ilkay Gundogan? Watatu hawa kwa pamoja na
 Bastian Schweinsteiger walikuwa ni baadhi ya viungo 
wangu bora wa ulaya msimu uliopita. Vipi kwa sababu 
hawana mpira wa madoido kiasi cha kushindwa kuingia 
mchuano wa kupigiwa kura kwa ajili ya tuzo hii? Listi 
iliyotolewa ni listi ya washambuliaji tu na wafungaji na
 matokeo yake tuzo hizi zimeonekana kuangalia 
vilivyovutiwa zaidi. 
  
Lakini haipaswi kuwa namna hii. Mshindi wa tuzo 
anabidi kuwa mchezaji ambaye amesaidia kuipeleka
 timu yake hatua nyingine ya ubora na mafanikio kwa 
maana ya vikombe.  Kwa maana hiyo inabdi mchezaji 
huyo atoke Bayern Munich. 

Bayern walikuwa bora na walitawala msimu uliopita na 
hii tuzo inabidi kuwa zawadi ya mafsnikio yao. Dortmund 
pia walikuwa bora lakini Bayern walikuwa zaidi. Heynckes
 inabidi awe kocha bora wa msimu na mchezaji wa Bayern 
atwae tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa ulaya na dunia. 
Lakini nani anastahili tuzo hizo? 
  
Kuna vipaji vingi sana katika kikosi cha Bayern; Lahm,
 Schweinsteiger na Javier Martinez wanastahili japo 
kutajwa kwa pamoja na Mandzukic. Klabu ilishinda makombe
 matatu - ni mafanikio ya timu kwa ujumla. Japokuwa, 
ikiwa utataka kumpa tuzo ni mchezaji mmoja binafsi 
katika wachezaji wa Bayern - basi  Frank Ribery anastahili 
tuzo hiyo mbele ya wengine na hizi ndio sababu kwanini 
anastahili.
  
Kutothaminiwa kwa Kipaji cha Ribery


Kutothaminiwa au kukubalika kwa mchango wa baadhi
 ya wachezaji bora kabisa linanikera sana. Sijui ni kovu
 lilo kwenye uso wake ambalo inawezekana ndilo 
linalowatisha au kesi yake inayomkabili kutembea 
kahaba aliye na umri mdogo, au mashabiki na vyombo 
vya habari hawaoni tu ubora alionao Ribery. Lakini kwa 
hakika kutokana kiwango chake msimu uliopita lazima 
watakuwa wameona ubora wa mfaransa huyu. 
  
Ribery alijiunga na Bayern mwaka 2007 akitokea 
Marseille kwa ada iliyoweka rekodi ya uhamisho 
wakati kwa klabu hiyo €25m. Hii ilikuja baada ya 
Zinedine Zidane kumpachika Ribery ‘mgodi wa madini 
wa soka’. Mambo mazuri zaidi yalitegemewa kutoka 
mfaransa huyu ambaye maisha yake ya soka yalitawaliwa 
na vizingiti vingi. 
  
Alifukuzwa kwenye academy ya Lille akiwa na miaka 16
 kwa kushindwa kufanya kazi za shule kitu ambacho kwa 
mujibu wa wanafunzi wenzie kilikuwa bora kwao kwa 
sababu walichoshwa na tabia yake ya ubabe. Aliendelea
 kujifunza soka na kucheza kwenye vilabu vidogo vidogo
 kabla ya kuhamia Metz. Kutokea hapo nyota yake ikaanza 
kupata mwangaza na kuvivutia vilabu kadhaa vikiwemo 
Galatasary na Marseille lakini mwishowe alibaki Ufaransa. 
Hapa ndipo aliporudi kwenye mstari - labda mafundisho
 aliyoyapata baada ya kusilimu na kuwa muislamu yalimtuliza
 mnamo mwaka 2006. 
  
Katika misimu yake miwili ya kwanza akiwa na Bayern Ribery
 alishinda tuzo ya mchezaji bora wa Ufaransa mwaka 2007 na 
2008 na pia alishinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Ujerumani 
 2008. Lakini kwa bahati mbaya majeruhi yakamharibia safari yake
 ya kwenda kuwa mmoja wa wachezaji bora duniani.
  
Lakini misimu miwili iliyopita, akiwa chini ya uangalizi wa 
Jupp Heynckes, ubora wa Ribery umeonekana dhahiri na 
muhimu zaidi kwa Bayern na mafanikio ya timu hiyo. Kwa 
kifupi kuibuka kwa Bayern na kuwa bora barani ulaya 
kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na Ribery ambaye hana 
mpinzani katika kikosi chake.
  
Hivi karibuni Joachim Low, kocha mkuu wa Ujerumani 
alikaririwa akisema kwamba Ribery ndio mchezaji bora wa 
soka la Ujerumani, akisisitiza kwamba uwezo wake wa kukaba 
na kushambulia hakuna mfano wake. 
  
Ubora wake katika kuzuia na kushambulia.
  
Ni vigumu kupingana na maoni ya Low kuhusu mfaransa 
huyu. Ribery amekuwa winga/mchezaji bora wa upande wa
 kushoto duniani kwa sababu ya uwezo wake wa kufanya kila 
kitu katika upande huo wa uwanja; akiwa anamiliki mpira 
anaweza kukimbiza ndani na nje na kutafuta nafasi ya kutoa 
krosi au kupiga mkwaju golini. Anaweza kuingia ndani na kucheza
 kwenye mstari na kuwa mchezeshaji pamoja na kufunga mabao pia.
 Japo hana uwezo wa kuchezea mpira kumzidi Ronaldo lakini
 kwa namna anavyoshambulia ni wachache sana wanaweza 
kucheza vizuri dhid yake. Na hapa akiwa anashambulia. 
  
Akicheza kama mlinzi basi labda hakuna mshambuliaji 
anayeweza kuzuia kuliko Ribery. Na hii inatokana utayari
 na kujituma kwake kufanya kazi ya kuzuia - kitu kinachomfanya 
kuwa bora zaidi kwa wakati huu. Nguvu na akili anayotumia 
inamfanya awe mchezaji sana kumtazama. Sio mbinafsi na 
utayari wake wa kufanya kazi kwa ajili ya timu unampa ubora
 ambao wengi wanaukosa.
  
Kiufundi anaofa vitu vingi kwenye mchezo wake lakini
 bado ana ndihamu ya mchezo, huku akiwa na maamuzi
 mepesi na sahihi kwenye mechi - kwa namna ya wapi na 
muda gani anatakiwa kuwa eneo lipi dimbani. Uwezo wake
 umetoa mchango mkubwa katika kuifanya Bayern iwe hapa
 ilipo sasa.

  Uwezo wa Frank Ribery ndio unawakilisha mchezaji wa 
kisasa anayehitajika kwenye soka la kileo. Hakuna nafasi 
ya kubaki nyuma au mbele pekee. Jukumu la mchezaji wa 
kisasa ni kuwa vizuri kwenye kushambulia na kuzuia. 
Ribery anaifanya yote haya kwa ubora wa hali ya juu na 
anastahili kutunzwa - UEFA na FIFA watakosa cha kujitetea 
safari hii kama tuzo zitaenda kwa mtu mwingine tofauti na 
Ribery. 

No comments:

Post a Comment