Vilio vingi vya wamiliki wa magari kwa sasa sio kuibiwa gari bali ni kuibiwa kifaa cha gari kinachotumika kupandishia vioo na kufungulia vitasa vya milango, ni kifaa ambacho kwa jina la kitaalamu kinafahamika kama "POWER WINDOWS".
Kama kunafasheni ya wizi basi naweza kuiita hii ni ya kisasa zaidi, kutokana na tabia hii ya wizi wa Power Windows kushamiri hasa katika maeneo ya mijini. Kipindi cha nyuma wadokozi hawa walionekana kujikita katika wizi wa redio za magari, lakini sasa wamegeuzia nguvu yao yote katika wizi wa Power Windows.
Hii ni tahadhari kwa wale wenye magari kuwa makini na udokozi huu ambao ukijipindua dakika tano tu mbali na upeo wa gari lako, basi umelizwa Power Windows au Side Mirror. Lakini tatizo hili sidhani kama litakwisha kwa haraka kama wauzaji spear za magari wataeendelea kununua vitu vidogo vidogo kutoka kwa watu ambao wanajua kabisa ni wadokozi.
Leo unaibiwa kifaa cha gari unaenda kununua kifaa hicho hicho kilichodokolewa kwa watu wengine, mimi nafikili wauza spear used au second hand za magari, mnapaswa kuwa waangalifu kwa hili.
No comments:
Post a Comment