aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, August 20, 2013

MAJAMBAZI YAVAMIA KITUO CHA MAFUTA KIBAHA....


ZAIDI ya watu 10 ambao wanadaiwa kuwa ni majambazi, wakiwa na mapanga na marungu, wamevamia kituo cha mafuta cha Derina Petrol Station, kilichopo Kibaha Picha ya Ndege, mkoani Pwani na kupora Sh milioni 15 na vinywaji mbalimbali vilivyokuwepo katika Super Market ya kituo hicho. 
Majambazi hayo yanadaiwa kuvamia kituo hicho kinachomilikiwa na David Mosha, saa saba usiku ambapo yalifanya fujo kwa kutumia silaha za jadi, hali iliyowafanya wafanyakazi wakimbie.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei, alisema majambazi hao walifika katika kituo hicho wakiwa na magari mawili, moja ni Prado na jingine Saloon yenye rangi nyeupe, ambayo yote yaliegeshwa karibu na pampu za kuwekea mafuta.

Alisema kuwa, baada ya magari hayo kusimama, majambazi hao wakateremka na kumkamata mfanyakazi wa zamu aitwaye Samson Rufunga (33) na mlinzi wa kituo hicho, Mohamed Shaban (47).

Kamanda Matei alisema baada ya kukamilisha kazi hiyo, majambazi hayo yaliwafunga kamba za miguu na mikono wafanyakazi hao na hatimaye kuwafungia ndani ya chumba kimoja kilichopo katika kituo hicho.

Watu wengine waliokamatwa ni pamoja na Frank Nyamahaga (28), ambaye ni dereva mkazi wa Tabata, ambaye walimpora Sh 100,000 na funguo ya gari yake aina ya Scania iliyokuwa imeegeshwa kituoni hapo.

Mwingine aliyekamatwa na kuporwa ni Isack Silinu (25) ambaye alikuwa utingo wa Scania hiyo mkazi wa Ipogoro, Iringa, ambaye naye aliporwa simu na fedha taslimu.

Wengine waliporwa katika kituo hicho ni Issa Mohamed (25), mfanyabiashara mkazi wa Frelimo Iringa, ambaye aliporwa simu ya Nokia yenye thamani ya Sh 75,000 na pesa taslimu Sh 68,000, wote walikuwa wakisafiri katika lori.

Mbali na hao, lakini Juma Selemani (30) ambaye ni dereva wa pikipiki mkazi wa Mwanalugali Kibaha ambaye alikwenda kituoni hapo kwa ajili ya kununua mafuta aliporwa pikipiki yake aina ya SANLG na fedha taslimu Sh 4,600.

Hata hivyo katika tukio hilo hakuna mtu aliyejeruhiwa, lakini Jeshi la Polisi mkoani Pwani linaendelea na jitihada za kuwasaka majambazi hao ili waweze kutiwa nguvuni.

No comments:

Post a Comment