aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, August 19, 2013

BIBI HARUSI MTARAJIWA AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI MASAA TU KABLA YA HARUSI YAKE,MARAKWET.....


Bibi harusi mtarajiwa alipigwa risasi na kufariki ijumaa jioni na majambazi pamoja na mdogo wake wa kiume kwa sababu zisizojulikana.

Mwanamke huyo mwenye miaka ishirini na kitu ilikuwa aolewe wikendi iliyopita Marakwet.

Mshuhudiaji wa tukio hilo alisema kuwa majambazi hao walikuwa watano walivamia nyumbani kwa wazazi wake kijiji cha Kapyego. Wakamshinikiza  mdogo wake wa kiume  kutaka kumuona dada yake,bibi harusi mtarajiwa.

Alisita na majambazi hayo walimpiga risasi akafariki hapohapo. Wakaingia ndani na kumtoa dada yake kisha wakampiga risasi kichwani.

Kiongozi wa polisi wa eneo hilo,Philip Opiyo aliyethibitisha kutokea kwa tukio hilo alisema kuwa mauaji hayo yanaweza kuwa yalisababishwa na 'love triangle'yaani akimaanisha mahusiano ya kimapenzi ya mwanaume mmoja kuwa na wanawake wawili. Polisi wana shuku kuwa mwanaume ambaye alitaka kumuoa  ndio anahusika na uvamizi huo.

Hata hivyo uchunguzi umeanza ili kujua hasa lengo la mauaji hayo...

Translated from DAILY POST

No comments:

Post a Comment