aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, August 17, 2013

AUAWA NA NDUGUZE KWA TUHUMA ZA UBAKAJI...


WATU wanne wamefariki dunia mkoani mbeya katika matukio tofauti, likiwemo la mfugaji aliyeuawa na nduguze kwa tuhuma za ubakaji.
Aliyeuawa katika tukio hilo lililotokea Agosti 14 mwaka huu saa tisa usiku katika kijiji cha Mabadaga wilayani Mbarali ametajwa kwa jina la Doto Sodela (26), Msukuma, mkazi wa kijiji hicho.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Diwani Athumani alisema Agosti 13 majira ya saa 10:30 jioni kijana Doto alitaka kumbaka binti Wayaga Mwinanira (14) ambaye pia ni nduguye aliyekuwa akichunga ng’ombe porini lakini hakufanikiwa.
Kamanda Athumani alisema baada ya wanandugu kupata taarifa hizo mnamo majira ya saa 5:00 walikusanyika nyumbani kwa kijana huyo kwa lengo la kumkamata lakini alipoonekana kuwa mbishi walianza kumshushia kipigo hadi pale mmoja wao alipompiga fimbo kichwani na kusababisha afariki papo hapo.
Alisema kutokana na tukio hilo, wanandugu watano wanashikiliwa na jeshi hilo ambapo aliwataja kuwa ni pamoja na Muondela Jinai (30), Shigela Sodela (33), Gere Mwinanira (39), Moshilo Mwinanira (22) na Vengo Sodela (29) wote wakazi wa kijiji cha Mabadaga.
“Tunaendelea na taratibu mbalimbali za kisheria ili watuhumiwa wafikishwe mahakamani. Kwa upande wa mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na tayari tumewakabidhi wanandugu kwa ajili ya maziko,” alisema.
Katika tukio la pili ni ajali iliyotokea juzi saa 2:30 usiku katika kijiji cha Chimbuya wilayani Mbozi katika barabara ya Mbeya-Tunduma ambapo gari lenye namba T 765 BBA aina ya Scania lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Tunduma likiendeshwa na dereva asiyefahamika lililigonga trekta lisiyofahamika namba za usajili kisha kuligonga Scania jingine mali ya kampuni ya Dhando lililokuwa likitokea Tunduma kuelekea Mbeya ambapo pia dereva hafahamiki.

No comments:

Post a Comment