MKAZI wa Kijiji cha Kanga wilayani Chunya mkoani Mbeya, Maria Martin (37),ameuawa kwa kupigwa ngumi kichwani na kukabwa shingoni na mpenzi wake kutokana na wivu wa kimapenzi.
Kwa mu j i b u wa t a a r i f a iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Diwani Athumani ilisema mkazi huyo alipatwa na mauti hayo Agosti 13, mwaka huu saa 6.05 usiku.
“Mtuhumiwa alifahamika kwa jina la Lameck Msangawale (35) ambaye alikimbia mara baada ya tukio kutokea,”ilisema taarifa hiyo.
Taarifa ilifafanua zaidi kuwa chanzo cha mauaji hayo ni kutokana na wivu wa kimapenzi baada ya mtuhumiwa kumkuta marehemu akiwa na mwanaume mwingine.Kamanda Athumani ametoa rai kwa mtu yeyote mwenye taarifa juu ya mahali alipo mtuhumiwa kutoa taarifa katika mamlaka husika ili sheria ifuate mkondo wake.
Katika hatua nyingine, mkazi wa Mbozi mkoani Mbeya, Sijaona Haonga mwenye umri wa miaka 45 ameuawa kwa kunyongwa shingoni kisha kutupwa kwenye mto unaojulikana kwa jina la Mlowo na watu wasiojulikana.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda Athumani ilisema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni kutokana na mgogoro wa mashamba ambapo ulitokea kati ya marehemu na Shabani Mbwili ikiwa ni pamoja na Mawazo Mbwili ambapo walitoroka mara baada ya tukio. Taarifa ilifafanua zaidi alisema mbinu iliyotumika kumuua marehemu aliviziwa wakati akivua samaki ambapo pembeni ya mwili wake kulikutwa ndoano ya kuvuliwa samaki.
Aidha mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi na daktari ikiwa ni pamoja na kuukabidhi kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya taratibu za mazishi. Kamanda Athumani alitoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi badala yake kuitatua migogoro yao kwa njia ya mazungumzo ili kuepusha mauaji yanayoweza kuepukika.
No comments:
Post a Comment