Picha juu na chini ni Washiriki wa Taji la Miss Universe 2013 wakipita jukwaani na mavazi ya ufukweni yaliyotengenezwa na Vitenge vya Polytex vinavyozalishwa na kampuni ya MeTL Group.
Walimbwende waliofanikiwa kuingia kumi bora wakipozi kwenye picha ya pamoja.
Warembo waliofanikiwa kuingia Top Five ya Miss Universe 2013.
Majaji wakiwa kwenye wakati mgumu wa kutafuta mshindi.
Kikundi cha sanaaa cha Haba na Haba kikitoa burudani wakati wa shindano hilo.
Miss Universe Tanzania 2012 Winfrida Dominique akipita jukwaani kuaga mashabiki.
Muandaaji wa mashindano ya Miss Universe Maria Sarungi Tsehai akimvalisha Taji Miss Earth 2013 Clara Noor.
Top Five ya Miss Universe 2013.
Mshindi wa Taji la Miss Universe Tanzania 2013, Betty Boniface (wa pili kulia), Miss earth Tanzania 2013, Clara Noor (wa kwanza kushoto) na Aziza Victoria ambaye ni mshindi wa pili (wa kwanza kulia) wakiwa kwenye picha pamoja.
Miss Universe Tanzania 2013, Betty Boniface (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Utalii kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Ibrahim Mussa (wa pili kushoto). Wengine katika picha ni Miss earth Tanzania 2013, Clara Noor (wa kwanza kushoto) na Aziza Victoria ambaye ni mshindi wa pili (wa kwanza kulia).
Mwakilishi kutoka SIA Couture akimkabidhi zawadi Mshindi wa Taji la Miss Universe 2013 Betty Boniface.
Meza kuu ya majaji.
Picha juu na chini ni baadhi wadau wa masuala ya urembo.
Na Mwandishi wetu
Betty Boniface (20) wa Dar es Salaam usiku wa kuamkia jana alifanikiwa kushinda taji la Miss Universe Tanzania katika mashindano yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini.
Mashindano hayo yaliyoshirikisha jumla ya warembo 15 kutoka mikoa nane ya Tanzania Bara, yalikuwa na ushindani mkali na Betty kufanikiwa kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Miss Universe ya kimataifa yaliyopangwa kufanyika mjini Moscow, Russia Novemba 9 mwaka huu.
Mbali ya nafasi ya kuiwakilisha nchi, Betty alipata zaidi ya Sh milioni 3 taslim na zawadi nyingine zenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 4.
Ushindani ulikuwa mkubwa katika mashindano hayo ambapo Clara Noor kutoka Mwanza alishinda taji la Miss Earth Tanzania na kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa nchini Philippines Novemba 3 mwaka huu.
Mrembo kutoka Dar es Salaam, Aziza Victoria alishinda nafasi ya pili katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na TANAPA, Fastjet, Mohamed Enterprises (MetL) na wadhamini wenza, Coca-Cola, Missie Popular Blog, Healthy Beauty Clinic, Beauty Point, Sia Couture, Seif Kabelele Blog, AZH Photography.com na Adams Digicom.
Betty alisema kuwa hakubahatisha kushinda nafasi hiyo kwani alijiandaa sana na lengo lake kubwa ni kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa.
“Nilijiamini kuingia katika mashindano haya, namshukuru Mungu kutimiza ndoto yangu, hivyo nitafanya zaidi ya Flaviana Matata mwaka 2007 nchini Mexico kwa kuingia zaidi ya hatua ya sita bora,” alisema Betty.
Muandaaji wa mashindano hayo, Maria Sarungi Tsehai alisema kuwa ushindani ulikuwa mkubwa na wanashukuru kufanikisha mashindano hayo huku hakiwashukuru wadhamini kwa msaada wao.