aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, August 18, 2013

Wajinga ndiyo waliwao! Baada ya Kilimanjaro, sasa wanatumia jina la Tanzania

Baada ya kupiga kelele kwa muda mrefu kuhusu vitabu, vijarida na vipeperushi vyenye picha ya Mlima Kilimanjaro ambapo hutumiwa jina lake kuvutia watalii kwa manufaa makubwa ya nchi jirani, leo hii mdau mmoja wa wavuti.com ameshangazwa na alichokikutda katika maduka ya bidhaa.

Alikwenda kwenye supamarkiti moja kwa ajili ya kununua bidhaa za Kitanzania (made in Tanzania) kwa minajili ya kupeleka zawadi kwa marafiki zake huko ng'ambo kwa kujivunia Utanzania na kuzitangaza bidhaa za nchi yake, kuwavutia wanunue bidhaa ili mwishowe mjasiriamali Mtanzania anufaike.

Ndipo katika kukagua aina mpya ya majani ya chai ili apate maelezo kwa muhtasari (kwa mfano apate majibu ya papo kwa hapo endapo ataulizwa chai hiyo inalimwa wapi, jiografia ya eneo, kampuni/ushirika unaozalisha), akaziona aina nyingi zenye chapa ambazo zilimkera, akakinai ndipo akatutumia picha hizi.
Picture
Picture
Picture
Maswali ya kujiuliza:

  • Hili ni kosa la bahati mbaya la kunakili na kubandika bila kusoma au ni kosa la makusudi kwa sababu hakuna anayejali? Kwamba aliyelala usimwamshe, mfaidi mjinga huyo!
  • Kuna kibali hutolewa na kupewa kisheria mtu kutumia jina la nchi nyingine kuuza bidhaa zilizotengenezwa kutoka nchi nyingine? Mathalan, unaweza kutumia America Safari Tea finest quality Tanzanian tea?

  • Tumelala! Tunayo mashirika mangapi yenye wafanyakazi wanaolipwa kwa ajili ya kukagua bidhaa na kulinda wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara, wajasiriamali na soko la Watanzania?

  • Ni kiasi gani cha mapato kinawafaidisha washindani kwa ulaghai wa kutumia jina la Tanzania?

  • Ni Watanzania wangapi bidhaa zao zinakosa nafasi kwa kuwa zimezidiwa na wingi wa bidhaa za kigeni?

wavuti.com na mdau wake tumefanya sehemu iliyo ndani ya uwezo wetu kwa kuanika hapa, huenda tukawa tumekosea, hivyo tuelimishwe ama huenda ni kosa kama tulivyoona, hivyo wahusika wachukue hatua.

Matumaini ni kuwa katika watembeleaji na wasomaji wa wavuti.com yupo anayehusika moja kwa moja katika hili au atakayeliona na kulisogeza panakohusika.


Source: wavuti.com

No comments:

Post a Comment