aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, August 18, 2013

WABUNGE WAAZIMIA KUTOTAJWA KWA RUSHWA....

                       Naibu spika wa bunge Job Ndugai

WA B U N G E wameazimia k u j i t a z a m a kuhakikisha mbunge hatajwi kwa rushwa wala uvunjifu wa maadili na Bunge linakuwa safi kabla ya kunyooshea vidole wengine.
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema azimio hilo limepitishwa na wabunge mjini hapa, kuwezesha Bunge kujitakasa na kuwa mfano wa kupambana na rushwa nchini. Kwa mujibu wa Ndugai, suala la maadili kwa wabunge, viongozi wa serikali na wa dini ni changamoto kubwa inayolikabili taifa.
Alisema hayo jana wakati akifunga mafunzo ya wiki moja kwa wabunge, ambao ni wajumbe wa Kamati za kusimamia fedha za umma na Bajeti, mjini Bagamoyo.
Mafunzo hayo yaliandaliwa na Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Katika mafunzo hayo, ambayo Naibu Spika pia alikuwa mshiriki, alisema suala la maadili na rushwa limezungumzwa na kujadiliwa kwa kina na kubaini kuwa ni tatizo kubwa nchini.
Alisema, “tumeona kabla ya Bunge kunyooshea wengine vidole, linapaswa lijitazame lenyewe na kuwa safi kwa kuhakikisha wabunge hawatajwi kwa rushwa na uvunjifu wa maadili kwa kuwa wao ni mfano kwa jamii.
Alisema, “Maadili ni eneo lenye matatizo mapana ndani ya nchi, sote tunahusika, wabunge wameona wazi huwezi kupambana na rushwa kama huna maadili, ni wito na azimio la wabunge hapa kwamba juhudi zianzie katika familia, lakini pia hata bungeni sisi wenyewe tunapaswa kujitazama kwanza tusitajwe kwa hili, ili tulisimamie.”
Ndugai pia alisema ni mapendekezo ya bunge kubadili mfumo wa ukaguzi wa hesabu za serikali na ufuatiliaji wa kamati unaofanyika baada ya fedha kutumika na kutumia pamoja na huo wa jumuiya ya madola, ule wa Bunge la Marekani.

No comments:

Post a Comment