aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, August 3, 2013

USHAWAI ZISOMA SIFA KUU 10 ZA RAIS WETU KIKWETE?? ZISOME HAPA



LT.DR.JAKAYA MRISHO KIKWETE:



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Rais mwenye sifa zifuatazo:-



1. Hachagui wala habagui ,amekuwa akijichanganya iwe kwenye



hafla,misiba,burudani nk bila ya kubagua.Mradi tu apatiwe mwaliko.



2. Hana kisasi na mtu,licha ya mengi ya ovyo ovyo kutolewa na wasio na mapenzi



naye amekuwa mwepesi kuyafunika na kuyaacha yapite kando yake.



3. Kwa uungwana wake,ameweza kuchagua hata mpinzani awe mbunge,hakika ni



kitendo cha ujasiri kufanya hivyo.Na hakijawahi kutokea katika historia ya kuanzia



Tanganyika hadi sasa Tanzania huru.Kama kimetokea basi nijuzwe.



4. Mkarimu na muungwana mwenye tabasamu muda wote.



5. Mkakamavu na mahiri katika kazi.



6. Asiyejali maneno zaidi ya utendaji kazi wa nguvu.



7. Rais pekee kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (haijawahi kutokea) kwa



kipindi cha utawala wake kutembelewa na marais/waziri wakuu wa nchi kubwa



duniani kwa kwa kipindi cha mwaka 1,katika ziara zao zenye manufaa kwa



watanzania.



8. Amesimamia kuziba ufa mkubwa wa kisiasa za kihafidhina kule Zanzibar kati ya



CCM na CUF na hatimaye kuundwa kwa serikali ya mseto iliyopo sasa madarakani.



9. Kwa kipindi chote suala la katiba limekuwa sawa na habari nyepesi nyepesi,lakini



kwake amelitimiza karibu 95% mpaka sasa.


10. Hana udini licha ya kuwa yeye ni mwenye imani ya dini ya kiislam.

No comments:

Post a Comment