aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, August 13, 2013

RONALDO AFUNGA AKIVUJA DAMU....!!


SUPASTAA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, ameripotiwa kuvumilia maumivu na kucheza akiwa anavuja damu mguuni ili tu amzibe mdomo kocha wake wa zamani, Jose Mourinho, aliyesema ovyo kuhusu yeye.

Mourinho alimponda Mreno mwenzake huyo kwamba si ‘Ronaldo halisi’ akimfananisha na fowadi wa zamani wa Brazil, Ronaldo de Lima.

Mourinho alitoa kauli hiyo siku chache kabla ya mechi baina ya Chelsea na Real Madrid iliyofanyika nchini Marekani, kitu ambacho Ronaldo alikuja kukijibu ndani ya uwanja kwa kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1 na hivyo kumfunga mdomo bosi wake huyo wa zamani.

Katika kutimiza lengo lake la kumzima Mourinho, Ronaldo alikumbana na vikwazo vingi uwanjani, ikiwamo kuvumilia maumivu baada ya kuonekana kifundo cha mguu wa kushoto kuvuja damu mchezoni.

Hadi filimbi ya mwisho katika mchezo huo, Ronaldo alimzima bosi wake huyo wa zamani.

No comments:

Post a Comment