aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 15, 2013

RIPOTI YA WIKI:VIROBA NDIO CHANZO CHA AJALI NYIGI ZA BODABODA....


RIPOTI ya Wiki hii imegundua kuwa ajali nyingi za pikipiki maarufu kama ‘bodaboda’ zinatokana na madereva wa pikipiki hizo kutumia vilevi vya kwenye pakiti maarufu kama viloba.
Uchunguzi umebaini kuwa, madereva wengi wa bodaboda hufanya kazi kwa muda mrefu bila kupumzika hivyo wanalazimika kutumia vilevi hivyo vya bei rahisi kwa kisingizio kuwa huondoa uchovu.
Katika hali hiyo, ajali nyingi huweza kutokea kwa kuwa vilevi hivyo hufikia hatua ya kumpotezea umakini dereva na kujikuta akiishia kusababisha ajali ambayo kama angekuwa hajalewa, asingeipata.
Ili kuthibitisha hali hiyo, Ripoti ya Wiki ilifanya mahojiano na baadhi ya madereva wa bodaboda ambapo wengi wao walikiri kutumia vilevi hivyo na kusema wanalazimika kufanya hivyo ili kuondoa uchovu kwa kuwa inawalazimu kufanya kazi kuanzia asubuhi mpaka usiku sana.
“Mimi binafsi natumia (anakitaja kilevi) ili kupoteza usingizi na uchovu. Lazima niwe macho usiku sababu abiria ndiyo huwa wengi muda huo,” alisema mmoja wa madereva hao aliyejitambulisha kwa jina la Hamisi Mbonde anayefanya shughuli zake maeneo ya Mbagala- Zakhem.
Aidha, Ripoti ya Wiki ilifanya mahojiano na trafiki mmoja wa makao makuu jijini Dar aliyeomba hifadhi ya jina lake na kusema kuwa mara nyingi madereva wengi wa bodaboda hasa wakati wa usiku hutumia vilevi hivyo na kubainisha kuwa ajali nyingi za pikipiki alizozishuhudia, zimetokana na madereva kuwa walevi.
“Mara nyingi kama ajali ya bodaboda imetokea, jambo la kwanza tunaloliangalia ni utimamu wa dereva ambapo tumegundua kuwa baada ya ajali, madereva wengi huonekana wamelewa,” alisema trafiki huyo.
Ripoti ya Wiki haikuishia hapo, ilifanya mahojiano na mtaalamu wa tiba na magonjwa mbalimbali, Dr. Richard Marise ili kubaini zaidi athari zitokanazo na kutumia kilevi hasa kwa madereva na kusema kuwa, kilevi cha aina yoyote huanza kwa kuchangamsha akili ya mtumiaji na baadaye kushambulia sehemu ya ubongo wa mbele na kumfanya mtu ashindwe kuona na kuzungumza  kisha kushindwa kuuendesha mwili wake, kabla ya kupoteza fahamu moja kwa moja.
 “Siyo vizuri kabisa kwa dereva kuendesha chombo akiwa amelewa kwa kuwa atajisababishia ajali na kugharimu maisha yake na ya abiria wake,” alishauri Dr. Richard.


No comments:

Post a Comment