aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, August 2, 2013

REAL MADRID NA MANCHESTER UNITED KWENYE MAZUNGUMZO YA KUMRUDISHA CRISTIANO RONALDO OLD TRAFORD

Real Madrid wapo tayari kumuuza Cristiano Ronaldo 
kwenda Manchester Unitedmwezi huu baada ya nahodha
 huyo wa Ureno kukataa kuanza mazungumzo ya mkataba
 mpya.

Gazeti la Daily Star limesema United na Real Madrid 
wametumia siku 12 zilizopita kuzungumza juu ya ada 
ya uhamisho ya paundi millioni 80 - na mabingwa wa 

Premier League wamezidi kupata uhakika wa kumrudisha 
kipenzi chao Old Trafford. 

Raisi wa Real Florentino Perez mwanzoni alitaka kwamba
 uhakika kutoka kwa Ronaldo kama yupo tayari kusaini 

mkataba mpya - na alishangazwa kwamba mchezaji kuwa 
alikuwa tayari kurudi United. 

Hilo lilipelekea Madrid kufungua mazungumzo rasmi 

na United, wakitambua kwamba wanaweza wakamuuza 
kwa fedha kidogo ikiwa winga huyo atabakia kwamwaka 
mmoja zaidi ndani ya Bernabeu kwa kuwa atakuwa 
amebakisha mkataba wa mwaka mmoja tu.  

Lakini pia imeonekana wazi kwamba Madrid wanataka
 kumpata mbadala wa Ronaldo - Gareth Bale ambaye 
tayari wameshatoa ofa ya £85m kwa Spurs.
Mapema wiki hii aliyekuwa raisi wa Madrid - Ramon 
Calderon alikaririwa akisema kwamba Madrid 
wanajiandaa kumuuza Ronaldo na ndio maana 
wanafanya kila liwezekanalo kumsajili Gareth 
Bale kutoka Tottenham.

Ikumbukwe pia wakati akiwa bado kocha wa Man 
United Sir Alex Ferguson alikarriwa akisema kila 
kipo sawa kwa ajili ya usajili wa mchezaji mkubwa 
wakati wa dirisha kubwa la usajili litakapofunguliwa.
 Pia Wakati akihojiwa na BBC hivi karibuni aliyekuwa 
msaidizi wa Ferguson - Mike Phelan aliulizwa kama boss 
wake alikuwa akimzungumzia Ronaldo aliposema kuhusu 
usajili wa mchezaji mkubwa? Phelan alishindwa kukataa wala
 kukubali kuhusu suala hilo, akisema "no comment'. 

No comments:

Post a Comment