aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, August 12, 2013

RAIS LUPOPO AMUITA KASEJA,PASSPORT YAKE YAIBWA...


KIPA wa zamani wa Simba, Juma Kaseja, ameendelea kukumbana na mikasa lukuki baada ya paspoti yake kuibwa katika hali ya utatanishi huku rais wa Klabu ya FC Lupopo, Victor Kasongo Ngoy, akimtaka aende DR Congo wiki hii.
Habari za uhakika zinaeleza kuwa, paspoti hiyo ya Kaseja iliibwa wakati akiwa kambi ya timu ya taifa hali iliyomlazimu kwenda kuripoti katika kituo cha polisi.
“Baada ya kutoa taarifa, Kaseja alianza kufanya mpango wa kupata pasi nyingine, kitu ambacho kiliwashangaza wengi ni kwamba chumba chake kilikuwa kimefungwa. Inaonekana kama kuna watu wanaomfuatilia.
“Maana walitaka asicheze mechi dhidi ya Stars, lakini hata yule wakala aliyetumwa na FC Lupopo kumfuata Kaseja, amekuwa akipata misukosuko kibao bila sababu, hali inayoonyesha kuna watu hawataki kuona anafanikiwa,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Alipoulizwa Kaseja kuhusiana na kupotea kwa paspoti yake, alisema yupo katika mikakati ya kupata paspoti mpya lakini akataka kuendelea kukaa kimya.
“Ni kweli, lakini ningependa niendelee kukaa kimya na mambo yaendelee yanavyokwenda,” alisema.
Taarifa nyingine zinaeleza, kipa huyo atasafiri kwenda DR Congo kuonana na rais wa timu hiyo kama atafanikiwa kupata haraka pasi hiyo ya kusafiria.
Kipa huyo amekuwa akiingia katika misukosuko mfululizo hali inayoashiria kwamba kuna watu walitaka kuona hachezi katika kikosi cha timu ya taifa na ikiwezekana asipate timu ya kuichezea.
Kaseja yupo katika hatua za mwisho za kusaini mkataba na FC Lupopo
.


No comments:

Post a Comment