aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, August 9, 2013

PICHA HALISI YA UJANGILI NCHINI....

 
Tembo akiwa amekufa katika moja ya Mbuga za wanyama nchini, huku meno yake yakiwa yameondolewa  

Wakati Taifa likididimia katika umaskini wa kutisha, wanyama ambao ni kitega uchumi cha nchi wanauawa kila siku na kundi la watu wenye uchu wa fedha. 
Tanzania ni nchi ya pili Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya tembo, baada ya Botswana.
Hata hivyo, ripoti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyama Pori (Tawiri), inaonyesha kuwa tembo 30 wanauawa kila siku katika mbuga mbalimbali hapa nchini.
Tawiri inaeleza kuwa miaka ya 60, Tanzania ilikuwa na tembo kati ya 250,000 hadi 300,000, lakini mpaka kufikia mwaka 2011, kuna tembo 70,000.
Utafiti uliofanyika umebaini kuwa upotevu huu wa tembo, unafanywa na genge la maharamia wenye mtandao uliojisuka hadi serikalini.
Imebainika kuwa mtandao huo ni mgumu kuuvunja kwani unahusisha wanasiasa, askari wa wanyamapori, polisi, mahakimu, raia wa nchi jirani, raia wa China, Thailand na Vietnam pamoja na wafanyabiashara wakubwa nchini.
Mara kadhaa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki amekaririwa akikiri kuwa ujangili wa pembe za tembo unahusisha mtandao mkubwa, wakiwemo wanasiasa.
“Kwa bahati mbaya sana, mtandao wa majangili wa pembe za tembo unahusisha wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa,” alisema. Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa baadhi ya watu wanaufahamu ukweli, lakini wanaogopa kuwataja wanasiasa hao kwa sababu za kiusalama.
Taasisi za wanyama pori zinashindwa kufanya kazi vyema na kuwataja wahusika wa genge hilo, kwa sababu wamo wanasiasa wakubwa.
Ripoti iliyosomwa bungeni hivi karibuni inaonyesha kuwa, baadhi ya makada wa CCM wanahusika katika ujangili wa pembe za tembo kwa kumiliki vitalu 16 vya uwindaji kinyume cha sheria.
Ripoti hiyo iliyosomwa na Chadema inamtaja mmoja wa mnakada wa chama tawala CCM, kuhusika na tuhuma za ujangili wa meno ya tembo katika ngazi za kimataifa.
Ilibainika kuwa kada huyo anamiliki kampuni za vitalu kwa majina tofauti, ili kuficha kuwa ni za mmiliki mmoja.

No comments:

Post a Comment