aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, August 10, 2013

Oprah Winfrey ‘Adhalilishwa’ Switzerland

Mwendeshaji wa kipindi cha ‘The Oprah Winfrey Show’, Oprah Winfrey
MWANAMKE maarufu duniani, Oprah Winfrey amekumbana na kitendo cha ubaguzi wa rangi nchini Switzerland baada ya muuza duka mmoja kukataa kumuuzia mkoba wa kike wa mkononi na kumwambia kuwa asingeweza gharama yake. Oprah ambaye ametajwa katika vitabu vya ‘Forbes’ kama mwanamke mwenye ushawishi mkubwa wa kisiasa duniani na mmoja wa watu matajiri zaidi amedai kuwa muhudumu wa kisichana aliyekuwa akiuza katika duka moja alimdharau kutokana na rangi yake.
Uswis imejikuta ikiwa gumzo kwa wanaharakati wa haki za binadamu, kwani wiki iliyopita nchi hiyo ilitangaza sheria kuwa wahamiaji wa nje hawataruhusiwa kushirikiana na raia wenyeji hasa katika maeneo ya umma kama vile mabwawa ya kuogelea, uwanja wa michezo na hata kanisani.
Sasa madai ya Oprah yanatoa taswira mbaya zaidi ya jinsi hali ilivyo nchini humo kuhusu ubaguzi wa rangi. Wanaharakati wa haki za binadamu wamesema kuwa hii ni ishara ya kuwa na ubaguzi ule uliowahi kutokea kwa muda mrefu huko Afrika Kusini. Oprah alisema aliamua kuondoka dukani hapo taratibu bila kufanya vurugu lakini amesikitishwa kuona kuwa bado ubaguzi wa rangi unaendelea na kuenea.
Mwaka jana pekee Oprah alikuwa na fedha jumla ya dola za Kimarekani milioni sabini na saba na amesifiwa kuwa mfanyibiashara tajiri, ambaye pia anamiliki shirika lake binafsi la utangazaji na anafadhili miradi mingi ya misaada katika maeneo anuai duniani.
Alipata umaarufu wake kutokana na kipindi chake cha Oprah Winfrey Show kinachooneshwa nchi nyingi. Hata hivyo mwandishi wa BBC mjini Zurich anasema kuwa kipindi hicho hakijawahi kupeperushwa katika runinga za Switzerland na huenda sio wengi wanaomfahamu Oprah ni nani. Oprah alikwenda Uswis kuhudhuria harusi ya mwanamuziki Tina Turner.
-BBC

No comments:

Post a Comment