aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, August 2, 2013

MREMBO SHINDANO LA MISS AFRICA AUAWA KWA KUCHOMWA VISU...

Lina Keza 
Mrembo chipukizi amekutwa amekufa kwa kuchomwa 
kwa visu huku binti yake wa miaka mitatu 'akilia pembeni 
yake kwenye dimbwi la damu', wamesema marafiki jana.

Mwili wa Linah Keza, mwenye miaka 29, ambaye 

inafahamika alishiriki kwenye Shindano la 
Miss Africa 2010, ulikutwa kwenye ghorofa moja 
huko King Edward Road, Leyton, juzi mapema
 asubuhi.
Tukio hilo liliripotiwa kwenye Tume Huru ya Polisi 

ya Malalamiko, ambayo itatazama mawasiliano yake 
waliyokuwanayo polisi na mwanaume mwenye miaka 
38 ambaye amekamatwa kuhusiana na kifo chake.
Madaktari wa Huduma za Gari la Wagonjwa London 

waliongozana na polisi kwenda mahali hapo kabla ya 
Saa 10:30 alfajiri, lakini Linah, raia wa Rwanda 
anayeishi London, alikuwa ameshatangazwa 
kufariki eneo la tukio.
Inafahamika kwamba binti yake alikuwa mahali 

hapo wakati wa shambulio hilo, kwa mujibu wa 
fafiki mmoja wa familia hiyo.
Herbert Muhire alisema: "Binti (yake) amepelekwa 

kwenye uangalizi na kupatiwa tiba ya kisaikolojia na
 matukio mengine baada ya kukutwa akilia kando ya 
mama yake huyo aliyekuwa amelala kwenye dimbwi 
la damu.
"Familia na marafiki wameelezewa jinsi alivyokuwa 


ameuawa na kufa kifo cha kutisha.
Rambirambi kwa Linah kutoka kwa marafiki na jamaa 

ziliachwa kwenye ukurasa wa Facebook uliofunguliwa 
mara baada ya kifo chake.
Azun Jezan aliandika: "Huzuni mno, roho yake ilale 

mahali pema peponi na binti yake na familia wajazwe 
nguvu katika wakati huu mgumu wa huzuni."
Mwingine, Justine Twongyeirwe, aliandika: "Nitakumbuka 

tabasamu lako mpenzi Linah. Ulale Mahali Pema."
Jana asubuhi, ukurasa huo ulikuwa na wafuasi zaidi 

ya 500 na baadhi walituma picha za Linah, ambaye 
alifanya kazi kama mrembo na kusomea huduma za 
jamii kwenye Chuo Kikuu cha Wolverhampton.
Kwa mujibu wa polisi, mwanaume huyo mwenye miaka 

38 alikamatwa baada ya kujisalimisha mwenyewe kwenye
 kituo cha polisi cha north London juzi.
Msemaji wa polisi alisema: "Uchunguzi wa mauaji

 umeanza baada ya mwanamke huyo kushambuliwa 
huko Leyton.
"Polisi waliitwa na Huduma za Gari la Wagonjwa 


London majira ya Saa 10:29 alfajiri ya Jumatano
 kwa ripoti za kuchomwa kwa visu.
"Maofisa na Huduma za Gari la Wagonjwa walifika 

na mwanamke huyo mwenye miaka 29 alikuwa 
ametangazwa kufariki kwenye eneo la tukio."
Uchunguzi wa mwili wake ulipangwa kufanyika 

majira ya Saa 5 jana asubuhi kwenye Mochari ya
 Walthamstow.

No comments:

Post a Comment