aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, August 10, 2013

MIILI YA POLISI WALIOGONGWA NA KUFA YASAFIRISHWA....


"MIILI ya askari wawili wa Kituo cha Polisi cha mjini Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Konstebo John Mkoma (26) mwenye nambari H1 na Benjamin Justine (27) mwenye nambari G 9696 imesafirishwa kwenda makwao kwa maziko. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alithibitisha leo kuwa, tayari miili hiyo ya askari hao vijana imesafirishwa jana jioni kwenda vijijini kwako kwa mazikom .
Aliongeza kuwa mwili wa Kontebo Mkoma umesafirishwa kwenda kijijini Msangano wilaya mpya ya Momba mkoani Mbeya ambapo mwili wa Konstebo Benjamin umesafirishwa kwenda kijijini Hedaru mkoani Kilimanjaro kwa maziko .
Kwa mujibu wa Mwaruanda askari hao walikufa baada ya kugongwa na gari linalodaiwa kuwa katika mwendo kasi Alhamisi wiki hii saa mbili za usiku usiku mjini Namanyere katika barabara ya kutokea Soko Kuu kwenda katika Kituo hicho cha Polisi kikazi .
Alibainisha kuwa ajali hiyo ya barabara ilihusisha pikipiki yenye namba za usajili T 903 DUP mali ya Mkoma aliyekuwa amempakia mwenzake, na gari aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T 875 CJC, mali ya Kaimu Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Nkasi, Simon Salala (31) ambaye ndiye aliyekuwa akiendesha gari hilo.
Akielezea tuko hilo, Mwaruanda alisema usiku huo polisi walikuwa wakielekea kazini, lakini ghafla waligongwa na Salala aliyekimbia na gari hadi nyumbani kwake na yeye mwenyewe kwenda kujificha,lakini baada ya msako alikamatwa na sasa na sasa anashikiliwa na jeshi polisi.

No comments:

Post a Comment