aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, August 20, 2013

MFANYAKAZI WA TANESCO AKAMATWA AKIIBA TRANSFOMA...


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia watu wawili, akiwamo mfanyakazi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), kwa tuhuma za kukutwa wakiiba transfoma kwenye ofisi za shirika hilo, Tawi la Magomeni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova, alisema  tukio hilo lilitokea usiku wa siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita, baada ya wasamaria wema kuitaarifu Polisi kuwa kuna mpango wa  wizi kwenye ofisi za shirika hilo.

Kova alifafanua kwamba ilipofika usiku Polisi waliliona gari lenye namba za usajili SU 37150 Toyota Dyna, likiingia kwenye ofisi za shirika hilo na baada ya muda waliwaona watuhumiwa wakipakia transfoma ya kwanza, kisha wakapakia ya pili na walipotaka kuipakia ya tatu ndipo polisi wakawavamia na kuwakamata watuhumiwa hao ambao aliwataja kuwa ni Daniel Milanzi (32) ambaye ni Dereva wa shirika hilo na Shukuru James (33) mkazi wa Buguruni.

Aidha Kamanda huyo alisema kuwa Polisi inalishikilia gari lililotumika katika wizi huo ikiwa ni pamoja na transfoma ambavyo vyote vimehifadhiwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay na uchunguzi kuhusu tukio hilo bado unaendelea.

Katika hatua nyingine wananchi wamewaua majambazi wawili baada ya kumpora mfanyabiashara mmoja Sh. milioni 28 eneo la Buguruni Malapa siku ya Jumapili.

Kamanda Kova alisema mfanyabiashara huyo, William Mathias, ambaye ni mkazi wa Kijitonyama aliporwa fedha hizo na majambazi hao ambao aliyataja kuwa ni Said Hemedi (42) mkazi wa Temeke na Robert Aloyce mkazi wa Mabibo, ambao walikuwa kwenye pikipiki mbili aina ya Boxer namba T 665 CJR na nyingine ambayo namba yake haikuweza kujulikana mara moja.

Alisema baada ya kufanikiwa kupora wananchi waliojitolea wakaanza kuwafujuza kwa pikipiki na  walipoona hivyo wakaanza kuwatupia wananchi fedha walizopora huku wakikimbia.

Kwa mujibu wa Kova majambazi hayo yalipofika Tazara yakakuta kuna Polisi ambao walikuwa wameshapata taarifa na kuweka ulinzi, hivyo kuamua kupunguza mwendo na wananchi hao wakawavamia na kuwapiga vibaya na kwamba walifariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali.

Alisema walikutwa na Sh. milioni 15 ambazo zilihesabiwa mbele ya mlalamikaji pamoja na bastola na bunduki
.

No comments:

Post a Comment