aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, August 5, 2013

MANCHESTER UNITED IMEACHANA NA MPANGO WA KUMSAJILI CESC FABREGAS - YASEMA FC BARCELONA


Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Barcelona sporting Andoni 
Zubizarreta amesema kwamba Manchester United imeachana na 
mpango wa kumsaini Cesc Fabregas.

United walituma ofa mbili zilizokataliwa na Barcelona kwa ajili 
ya kumsaini kiungo huyo mwenye miaka 26 na Barca wamekuwa
 wakirudia mara kwa mara kwamba hazuwi.

Huku kukiwa na tetesi kwamba United wanajiandaa kutuma 
ofa ya tatu, Zubizarreta ameliambia gazeti la Marca kwamba 
United wameachana na mpango wa kumsajili Cesc. 

"Manchester United wameonyesha kuvutiwa na mchezaji, lakini
 pia wameshaelewa kwamba hatutaki kumuuza.

"Wameshaondoa suala hilo mezani. Hatumuuzi Cesc Fabregas."

No comments:

Post a Comment