aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, August 17, 2013

KIWEWE,MATUMAINI WAOKOKA

Stori:Mayasa Mariwa
MSANII wa Kundi la Ze Komedi, Robert Augustino ‘Kiwewe’ na mwenzake Tumaini Martin ‘Matumaini’ wameamua kuacha anasa na kumrudia Mungu kwa kuokoka.
Wakizungumza na paparazi wetu kwa nyakati tofauti, wasanii hao walisema kilichosababisha kuchukua uamuzi huo kwa wakati mmoja ni kutokana na manzingira waliyolelewa tangu wakiwa wadogo, yaani kumjua Mungu.
“Niliamua kufanya uamuzi sahihi ambao naamini utanibadilishia maisha yangu kwa kiasi kikubwa, kwa kufuata mambo yanayompendeza Mungu na siyo starehe za ujana,” alisema Kiwewe huku akiungwa mkono na Matumaini. Wakabainisha kuwa wanasali kwa Mchungaji Josephat Gwajima.
Wasanii hao walisema, ili kuhakikisha wanaungana na Mungu katika kila jambo, wameamua kuanzisha kundi lao la muziki wa Injili, Comedians Gospel linaloundwa na wao pamoja na Mkono.

No comments:

Post a Comment