aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, August 19, 2013

KESI YA OSCAR PISTORIUS ALIYEMUUA MPENZI WAKE KWA KUMPIGA RISASI ITAANZA MACHI MWAKANI....

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amefika mahakamani ambapo ameshtakiwa kwa mauaji ya mpenzi wake.
Mahakama imemsomea makosa ya kumuua,Reeva Steenkamp. Kesi dhidi ya mwanariadha huyo itaanza Mwezi Machi mwaka ujao.

Oscar Pistorius alizingirwa na umati mkubwa wa waandishi wa habari alipofika mahakamani mji wa Pretoria. Akiandamana na jamaa wake mwanariadha huyo alifanya maombi maalum. Punde baada ya kusomewa makosa ya kumuua Mwanamitindo Reeva Steenkamp, Oscar alionekana kupatwa na huzuni kubwa.

Kesi hiyo sasa imehamishiwa mahakama kuu na itasikizwa mapema mwakani.Pistorioua anadaiwa kumpiga risasi mpenzi wake usiku wa manane akiwa amejifungia choo ya nyumba yake.
Mwanariadha huyo amejitetea na kusema alidhania ni mtu mwingine aliyejaribu kuingia kwa nguvu ndani ya nyumba. Upande wa mashtaka umesema mwanariadha huyo alipanga kumuua mwanamitindo huyo.

Mmoja wa majirani wa Pistorius na ambaye ni shahidi alikiri kusikia mayowe ya mwanamke huyo kisha milio ya risasi. Hata hivyo shahidi mkuu anayefahamu kilichotokea wakati huo ni mmoja tu naye ni Oscar Pistorius.

No comments:

Post a Comment