aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, August 10, 2013

Kapombe aichanganya Simba


Mashabiki wa timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam wakiishangili timu yao uwanjani 
KWA UFUPI
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema jana kuwa, AS Cannes imeonyesha kumtaka Kapombe, lakini amechelewa kwenye usajili, hivyo atalazimika kucheza kwa mkopo mwaka mmoja.

Dar es Salaam. Uongozi wa Simba umesema utafanya uamuzi mgumu kwa mchezaji wake Shomari Kapombe kwa kumruhusu kucheza kwa mkopo klabu ya AS Cannes ya Ufaransa, na kama atauzwa basi dau lake siyo dola 300,000.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema jana kuwa, AS Cannes imeonyesha kumtaka Kapombe, lakini amechelewa kwenye usajili, hivyo atalazimika kucheza kwa mkopo mwaka mmoja.
“Kama Kapombe angeenda Juni, ingekuwa rahisi kusajiliwa, lakini tumechelewa kumpeleka. Tatizo lingine, kiwango chetu Fifa (Fifa ranking) kuwa chini, kwani wenzetu Ulaya hawaangalii mchezaji mmoja mmoja.
“Sisi kama Simba itabidi tufanye uamuzi mgumu kwa wachezaji wetu, tutaanza na Kapombe, nadhani hili litasaidia kuwafungua hata wachezaji wengine.
Wachezaji wa Kenya na Uganda wanakwenda nchi kama Norway na nyingine, ambapo wanacheza kwa mkopo kisha ndiyo wanapata timu kubwa,” alisema Rage
Rage alisema kwa sasa wapo kwenye mazungumzo na klabu hiyo kuangalia ni namna gani watapata haki zao baada ya mwaka mmoja.
“AS Cannes wametutajia timu nyingi wanazoweza kumuuza Kapombe na klabu tukanufaika. Nimewapa masharti, watuhakikishie kama kweli watasajiliwa baada ya huo mwaka mmoja, na pia watuambie tutanufaika vipi,” aliongeza Rage.
AS Cannes iko daraja la nne, CFA, chini ya Ligue 1, Ligue 2 na National na ni timu kubwa, ndiyo iliyowatoa kina Patrick Vieira na Zinedine Zidane na katika majaribio yake aliyofanya amepangwa namba tofauti ikiwamo beki ya kati, kiungo na beki ya kushoto na ameonyesha kiwango kizuri.
Wakati huohuo, Simba itashuka dimbani leo kuikabili SC Villa ya Uganda, lakini habari mpya ni kuwamo kikosini kwa mara ya kwanza kwa nyota wake watatu wa kimataifa, Hamis Tambwe, Gilbery Kaze na Joseph Owino.
Mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki utaenda sambamba na sherehe maalumu ya ‘Siku ya Simba’ yenye lengo la kuwatambulisha wachezaji wapya.
Owino raia wa Uganda amejiunga na Simba akitokea klabu ya URA, wakati Warundi Kaze na Tambwe wamejiunga na wekundu hao wakitokea klabu ya Vital’ O
.

No comments:

Post a Comment