Muigizaji mkongwe wa filamu nchini, Issa Musa maarufu kwa jina Claudi amesema licha ya kuwepo kwa utitiri wa filamu za Tanzania sokoni, bado hakuna hata moja inayoweza kuitwa movie.
Sehemu ya cover la filamu aliyoigiza Claudi, Wrong Decision
Claud alikuwa akiongea Jumanne hii kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV.
“Tunafanya tu vitu vya kufanya watu watukubali wacheke majumbani kwao lakini bado Tanzania hatujatengeneza movie,” alisema.
“Na sababu yangu ya kusema kwamba hatujatengeneza movie, kuna wengine watacomplain ‘Claud anajidhalilisha’ hapana lazima tuzungumze ukweli. Ni kwamba haiwezi kuwa movie more advanced ikawa wewe kila kitu unafanya wewe, mengine utayaona wapi,” alisisitiza Claud kuzungumzia kasumba iliyopo kwenye kiwanda cha filamu Tanzania ambapo mtu mmoja hufanya kazi zote kuanzia kuigiza, kuandika filamu, kuongoza filamu na kutayarisha.
“Wasanii hasa sisi wenye majina, tukishafikia stage flani tunajiona tuna mashabiki wengi kwahiyo ina maana kwamba sis ndo tunajua kila kitu, kwamba sisi hatuwezi kukosolewa, hakuna mtu anaweza kutuambia kitu, kumbe mwisho wa siku ni sifuri. Hakuna mwanadamu mkamilifu.”
Hata hivyo Claud alisema kutokana na wasambazaji kuwapa bajeti ndogo ya filamu zao, wasanii hujikuta wakifanya kazi zote wao wenyewe ili kukwepa gharama.
“Mwisho wa siku najikuta sehemu zote nakaa mwenyewe kulinganisha na bajeti ninayoipata siwezi nikagawana na watu wote. Lakini kama bajeti ikiwa inatoka vizuri nakuwa na hela nzuri ya kumlipa director, nina hela nzuri ya kumlipa mtunzi mimi naishia kucheza tu.
Aidha Claud alisema soko la filamu la Tanzania huangalia ni kiasi gani movie inauzika na sio ubora wa filamu yenyewe.
SOURCE: BONGO 5
No comments:
Post a Comment