Mtoto Mesiah na mama yake
Kwa mara ya kwanza jaji Lu Ann Ballew huko Newport, Tennessee nchini Marekani amelazimika kuwaamuru wazazi wabadili jina la mtoto wao (miezi 7) kutoka Messiah na kuwa Martin kwa sababu za kiimani, akisema jina la Messiah linampasa mtu anayelistahili na mtu huyo ni Yesu Kristo, "the religious name was earned by one person and “that one person is Jesus Christ.”"
Kilichosababisha hata jaji Lu kufikia uamuzi huo ni baada ya wazazi hao kupelekana mahakamani kushitakiana kuhusu jina la mwisho la mtoto huyo, lakini kabla hata ya kuamua kuhusu jina la mwisho, jaji
alipotamkiwa jina la kwanza tu akaanzia papo hapo. Allisema mtoto huyo aitwe Martin DeShawn McCullough, jina ambalo linabeba majina ya mwisho ya wazazi wote wawili.
Jaji huyo alisema ameamuru jina la Messiah lisitumike ili kumwepusha mtoto na usumbufu anaoweza kuupata endapo ataishi katika miji yenye mizizi ya imani ya Kikristo ambapo jina/neno "Messiah" ni la heshima ya pekee kwa Masihi Yesu Kristo.
Mama wa mtoto huyo amesema atapinga uamuzi huo katika ngazi inayofuata ya mahakama kwa kuwa anataka jina la mwanaye Messiah lilandane na majina ya watoto wake wengine wawili -- Micah na Mason.
Messiah ni jina lililopendwa sana mwaka 2012 ambapo lilishika nafasi ya 4 katika majina pendwa mwaka huo (rejea: The Social Security Administration’s annual list of popular baby names).
--- Habari kwa mujibu wa The Associated Press, 2013.

No comments:
Post a Comment