aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 14, 2013

BATULI AANZA KUTEMBELEA MAGONGO BAADA YA KUUMIA AKIWA ANATENGENEZA FILAMU...

MSANII wa filamu nchini Zaytun Kibwana 'Batuli' sasa atembelea magongo baada ya kupata matibabu ya mguu baada ya kuumia akiwa anatengeneza filamu 'Location'.

Msanii huyo ambaye anashindwa kutembea au kujisogeza ameweza kupata matibabu kwa kuwekewa kifaa maalumu, kitakachoweza kurudisha goti katika hali ya kawaida. Akizungumza mara baada ya kuwekewa kifaa hicho chenye chuma, Batuli aliweka wazi kuwa ameanza kupata nafuu ingawa anatumia magongo kwa ajili ya kutembea na kusimama.

Alisema dokta ndiye aliyemshauri kutumia kifaa hicho kuliko kufanya upasuaji ambao ungempelekea kukaa kitandani kwa muda mrefu huku akishindwa kutembea.

No comments:

Post a Comment