aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, August 25, 2013

Askari wa JWTZ aliyetoroka ni mzaliwa wa Kagera; Uroro wake si tishio kwa Taifa

JESHI LA wananchi wa Tanzania (JWTZ), limetoa ufafanuzi kwa kusema kuwa askari wake aliyetoroka jeshini Luteni Kanali Coelestine C. Seromba kwa kusema kuwa ni mzaliwa wa Kagera na siyo Rwanda.

Jeshi hilo limevitaka vyombo vya habari kuacha kuripoti taarifa potofu za afisa huyo ambaye alikuwa akikabliwa na tuhuma za makosa ya kijeshi na baadaye akatoweka wakati mchakato wa kumfungulia mashitaka ukiendelea.

Msemaji wa Jeshi hilo Meja Erick Komba Tamba akizungumza na wanahabari Dar es Salaam siku ya Jumamosi, alisema Seromba alitoroka Desemba 17 mwaka jana baada ya kuona kosa lililokuwa linamkabili linaweza kumtia hatiani, hatua ambayo amesema haina madhara kwa jeshi hilo. Kwa kuwa Lut. Kan. Seromba alitambua kuwa ametenda kosa na kuamua kutoroka, hatua ambayo ni kinyume cha sheria za JWTZ, ataendelea kutafutwa na akipatikana, atafunguliwa mashitaka kwa kosa la kutoroka JWTZ.

---

Blog moja inasema kutokana na serikali kupenda kuajiri vyeti badala ya watu, kuna kundi kubwa la askari wa majeshi ya Tanzania ambao siyo raia wa nchi hii na inasisitiza kuwa imewahi kuripoti uwepo wa raia wa Rwanda na Burundi katika majeshi ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment