Ripoti kutoka Somalia zinasema kuwa wapiganaji wa kundi
la wanamgambo wa kiislamu la al Shabab wameanza
kupora kliniki zinazomilikiwa na shirika la kutoa msaada wa
kitabibu la Medicins Sans Frontiers, MSF, baada ya shirika
hilo kutangaza kuwa linajiondoa kutoka nchini humo.
Wenyeji katika eneo la Bay kusini magharibi wamesema
waliona wanamgambo wakipora madawa, kompyuta pamoja
na mitambo mingine kutoka katika makao makuu ya shirika
hilo.
Siku ya jumatano, shirika la MSF lilisema kuwa linasitisha
shughuli zake zote kufuatia mashambulizi ya mara kwa mara
dhidi ya wafanyikazi wake.
Tangu shirika hilo lianze kufanya kazi nchini Somalia mwaka
1991, wafanyikazi wake kumi na sita wameuwawa.
Wengine wawili walitekwanyara mwaka 2011 na kuachiliwa hivi maajuzi.
No comments:
Post a Comment