aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, August 3, 2013

Ajali yaua 2,yajeruhi 10 Morogoro

 Watu wawili wamefariki dunia  na kumi wamejeruhiwa baada ya gari aina ya pickup mali ya kampuni ya hood  iliyokuwa imebeba ndugu wa familia moja  wakielekea msibani  kuacha njia  na kupinduka mara tatu katika eneo la kata  ya mkuyuni wilayani morogoro .
Vilio na majonzi  vilitawala   katika hospitali  ya mkoa wa morogoro  mara baada  maiti na majeruhi  kuwasili
Ambapo ndugu wa marehemu wamesema  waliofariki ni  leila ngurungu  pamoja na kaka yake aliyekuwa mchezaji wa siku nyingi katika soka idrisa ngurugu  ambapo wamesema walikua njiani kwenda kwenye msiba wa kaka yao mkubwa  ambapo njiani walipata ajali na kuwa chanzo  cha ajali ni mwendo kasi  huku baadhi wa ndugu wakieleza  kuwa msiba huo ni pigo kwani wamepoteza ndugu watatu wa familia moja.
 Nao majeruhi  waliolazwa  katika hospitali ya mkoa wa morogoro wakiziungumzia tukio hilo wamesema chanzo cha ajali ni dereva wa gari aina ya pickup aliekua akijaribu kukwepa ajali ya uso kwa uso na kisha gari kuacha njia na kupinduka mara nne.
 Jeshi la polisi Mkoa wa morogoro limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na maiti zimehifadhiwa katika chumba cha maiti hospitali ya mkoa wa morogoro na majeruhi wanaendelea na matibabu

No comments:

Post a Comment