aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, November 30, 2013

Wananchi wa jiji la Arusha ambao ni wafuasi wa CHADEMA waandamana na mabango wakimshinikiza Godbless Lema ajiuzulu kwa kuwa jimbo limemshinda


Wafuasi wa CHADEMA jijini Arusha walioambatana na Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Monduli Bw. Amani Salenga wakionyesha bango hilo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani)..

Amani Salenga akiwa na kundi kubwa la vijana walikutana na waandishi wa habari na kudai kuwa Mbunge wa Arusha, Godbless Lema ndo chanzo cha vurugu ndani ya CHADEMA kwa kuanzisha kikundi cha vijana kinachohatarisha maisha ya wale wanaopinga na mawazo ya Lema katika utendaji wa chama mkoani Arusha.
 
Amani alisisitiza kuwa kwa kuwa CHADEMA  imeamua kufanya maamuzi kwa maslahi ya watu binafsi hususani swala la viongozi waliovuuliwa vyeo vyao(zitto),basi kila mwanachadema  anatakiwa atambue kuwa ndani ya chama hicho kuna pande mbili , CHADEMA ASILI na CHADEMA FAMILY.


Vijana hao waliokuwa na mabango mbalimbali wamelaani  hatua  ya  chama  chao  kuwafukuza  viongozi  wao  pasipokufuata  katiba  ya  chama  na kusisitiza kuwa Lema ndo tatizo ndani ya Chadema .

No comments:

Post a Comment