Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kimewaandikia barua za kuwavua rasmi nyadhifa za uongozi aliyekuwa naibu katibu mkuu Mh. Zitto Kabwe na wenzie sambamba na kupewa siku kumi na nne za kujieleza kwa nini wasivuliwe uanachama kufuatia waraka wa siri walioundika na kukamatwa hivi karibuni.
Mkurugenzi wa habari na uenezi Chadema Mh. John Mnyika amesema barua hizo zilizoainisha makosa kumi na moja ya kukiuka katiba na itifaki za chama hicho zitawataka wahusika kujieleze kwa maandishi na baadae mbele ya chama kwa nini wasifukuzwe na kuvuliwa uwanachama kufuatia waraka waliouandaa uliosemekana ulilenga kikupindua chama hicho.
Aidha Mh. Mnyika ameongeza kuwa waraka uliochapisha kwenye baadhi ya magazeti na mitandao mbalimbali ya kijamii sio ule uliowahukumu wahusika hao na kuwaomba watanzania na wafuasi wa chama hicho kutoutilia maanani waraka huo na siku itakapobidi kuutoa waraka husika watafanya hivyo.
Awali mwanasheria mkuu wa chama hicho Mh. Tundu Lissu akizungumzia mkutano uliofanywa na Mh. Zitto na wenzie licha ya kukata kusema hatua zitazozochukuliwa pindi watakaposhindwa kutimiza mashati waliyoyaweka amesema mkutano huo ulilenga kupoteza lengo kuu la kuvuliwa madaraka na kuwa kilichowafukuza ni mkakati wao wa siri uliolenga kukipindua chama hicho na si vinginevyo.
No comments:
Post a Comment